Na Baraka Mpenja
Wana
lambalamba, Azam fc yenye makazi yake Mbande Chamazi nje kidogo ya
jijini la Dar es salaam wamesema maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kesho
katika uwanja wa taifa dhidi ya Mgambo shooting ya Tanga yamekamilika
na wapo tayari kusaka pointi tatu muhimu ili kutetea umakamu bingwa wao
walioutwaa msimu uliopita.
Mechi
ya Azam dhidi ya Mgambo Shooting itachezeshwa na refa Jacob Adongo
kutoka Mara, na atasaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Charles
Mbilinyi wa Mwanza. Mwamuzi wa mezani atakuwa Idd Lila wa Dar es Salaam
wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.
Akizungumza kwa njia ya Simu na mtandao wa MATUKIO DUNIANI
kutoka Dar es salaam, Afisa habari wa klabu hiyo Jafar Idd Maganga
amesema kikosi kipo salama na wanamshukuru mungu kwa kuwajalia afya na
wanaendelea kumuomba ili awafikishe salama hapo kesho.
“Kila kitu
kipo tayari, maandalizi yamekamilika, wachezaji wana morali kubwa na
wameandaliwa vizuri na jopo la ufundi chini ya kocha wetu Muingereza
Stewart John Hall”. Alisema Jafar.
Jafar
alisisitiza kuwa japokuwa ushindani ni mkubwa sana kusaka nafasi ya pili
hasa baada ya waliokuwa mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita, wekundu
wa Msimbazi Simba kufanya vizuri na kuwapumulia kwa karibu hivi sasa.
“Sisi
tunataka kuliwakilisha tena taifa kwa mara nyingine katika michuano ya
shirikisho na kufika mbali zaidi ya mwaka huu ambao tumetolewa raundi ya
tatu, hivyo nafasi ya pili kwetu ni muhimu sana na tunajipanga kushinda
kesho ili kujiweka mazingirza ya uhakika”. Alisisitiza Jafar.
Azam yenye pointi 48 inahitaji pointi moja zaidi ili kutetea nafasi ya pili kwa mara nyingine.
Wakati
Azam ikisaka pointi hiyo moja, Mgambo Shooting inayofundishwa na
wachezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988, Mohamed
Kampira akisaidiwa na Joseph Lazaro ni moja ya timu ziko katika hatari
ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.
Mgambo
Shooting inahitaji pointi moja tu katika mechi mbili ilizobakiza
kukwepa kurudi FDL, ikishindwa kupata pointi hiyo huku Polisi Morogoro
na Toto Africans ya Mwanza zikishinda mechi zao za mwisho kwa uwiano
mzuri wa mabao itakuwa imekwenda na maji.
0 comments:
Post a Comment