Na Baraka Mpenja
Safari
ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, klabu ya
Azam fc yenye makazi yake Mbande Chamazi jijini Dar es salaam imeishia
mikokoni mwa waarabu wa Morroco, AS FAR Rabat baada ya kukubali kufungwa
mabao 2-1 huku Azam wakikosa penati dakika za lala salama za mechi
iliyopigwa katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat nchini
Morroco.
Wana
lambalamba hao wametoka kwasababu katika mchezo wa kwanza uliopigwa
uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita walitoka
suluhu pacha ya bila kufungana na leo hii wamefunga mabao hayo na kutoka
kwa wastani wa mabao mawili kwa moja.
Endapo Azam wangetoa sare yoyote ile wangesonga mbele katika michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini.
Azam
waliingia uwanjani kwa kujiamini na kupata bao la kuongoza katika dakika
ya 6 ya mchezo kupitia kwa John Raphael Bocco “Adebayor” na dakika sita
baadaye FAR Rabat wakasawazisha bao hilo.
Dakika
ya 43 Azam walifungwa bao la pili na la ushindi kwa wenyeji wao na
kuwaacha Watanzania wachache waliokuwepo huko wakiwa na butwaa baada ya
taifa kubaki bila timu katika michuano ya kimataifa.
Kipindi
cha kwanza kilimalizika kwa wenyeji kucheza pungufu baada ya mchezaji
mmoja kupewa kadi nyekundu kwa kosa la kumfanyia madhambi Brian Umony.
Kipindi
cha pili kipute hicho Azam walilazimika kucheza pungufu kipindi cha
pili baada ya walinzi wake David Mwantika na Waziri Omary kuoneshwa kadi
nyekundu kwa nyakati tofauti.
Matumaini
ya Azam kusonga mbele yaliongezeka katika dakika ya 81 baada ya
kuzawadiwa penati lakini Bocco alikosa mkwaju huo na kuwaacha mashabiki
wa soka Tanzania vichwa chini.
Kwa ujumla katika mchezo wa leo makosa ya mabeki wa Azam kukaba vibaya ndio chanzo cha kupoteza mchezo huo.
Pia
washambulaiji wa wana lambalamba hao wakiongozwa na John Bocco na Kipre
Herman Tchetche walipoteza nafasi za kufunga na wangeongeza umakini basi
wangeibuka kidedea na kuendelea kuwapa raha Watanzania.
AS
FAR Rabat walicheza soka la kasi licha ya kuwa pungufu, lakini
walipoteza nafasi nyingi na mashambulizi ya kushitukiza yalitawala kwa
timu zote.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao,
Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Kipre
Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba
dk79 na Brian Umony/Khamis Mcha dk70.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali Medamine na El Yousfi Mostafa.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali Medamine na El Yousfi Mostafa.
0 comments:
Post a Comment