Na Baraka Mpenja
Baada
ya kutolewa katika kombe la shirikisho barani Africa, klabu ya Azam fc
maarufu kama “Lambalamba” leo imesema kuwa sasa imerudisha akili yake
katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayoelekea ukingoni kwa
msimu huu wa 2012/2013.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga ameimabia MATUKIO DUNIANI kuwa
leo hii klabu hiyo inaingia kambini katika hosteli zao za Chamazi
Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa
jumapili dhidi ya maafande wa jeshi la kujenga taifa kutoka mkoani Pwani
Mgambo Shooting.
“Wachezaji
wote wamerudi salama baada ya kuhuzunishwa na matokeo ya Morroco,
lakini hili ndio soka, tunajua wazi kuwa matokeo yale yaliwashangaza
wengi hasa baada ya mchezaji wetu Bocco kukosa penati dakika za lala
salama, lakini soka lina mambo yake na sasa tunajiandaa na ligi kuu”.
Alisema Jafar.
Jafar
alisisitiza kuwa azima yao ni kushiriki kwa mara ya pili michuano ya
kimataifa mwakani na ndio maana wanaanza kampeni ya kuchukua nafasi ya
pili msimu huu kwa kushinda mechi zilizosalia.
Afisa
habari huyo alisema licha ya kutupwa nje na AS FAR Rabat ya Morroco
lakini wamejifunza mengi kwani wao bado ni wachanga sana katika
mashindano ya kimataifa kwani ndio kwa mara ya kwanza wameshiriki mwaka
huu.
“Kila
mtu ameona jinsi tulivyoonesha ushindani mkubwa kimataifa, tunataka
kupata nafasi nyingine msimu ujao ili tuwakilishe taifa kwa uzuri
zaidi”. Alisisitiza Jafar.
Azam
fc mpaka sasa wapo nafasi ya pili ya ligi hiyo wakijikusanyia pointi 48
huku nyuma yao wakiwemo simba wenye pointi 42 nafasi ya tatu na leo hii
wanashuka dimbani kumenyana na Mgambo Shooting ya Mkoani Tanga katika
uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment