Thursday, May 2, 2013


Fiti kabisa;Atudo mazoezini Rabat,
akituliza mpira kwenye bega lake,
kuashiria limepona kabisa

Na Mahmoud Zubeiry, Rabat
BEKI mahiri wa Azam FC, Joackins Atudo Otieno amesema kwamba sasa anajisikia vizuri kabisa na hahisi tena maumivu ya bega, yaliyomfanya akacheza kwa dakika saba tu mechi ya kwanza ya Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS FAR Rabat, Uwanja wa Dar es Salaam wiki iliyopita.
Na kuelekea mchezo wa marudiano Jumamosi, beki huyo wa kimataifa wa Kenya amesema kwamba yuko fiti kabisa kwa purukushani za aina yoyote kuhakikisha anaisaidia timu yake kushinda na kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Akizungumza mjini hapa jana, Atudo ambaye ni beki bora wa Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita alisema kwamba mapumziko ya wiki moja aliyoyapata yamemsaidia kupona maumivu ya bega na sasa anajisikia vizuri kabisa.
“Kwa kweli sasa hivi sisikii tena maumivu yoyote, bega liko poa na ninaweza kukandamizana sana tu, hii kupumzika imenisaidia sana,”alisema beki huyo mahiri, ambaye hupanda kusaidia mashambulizi na kufunga hadi kwa mipira ya adhabu. 
Beki huyo wa Harambee Stars, aliumia bega katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Pwani Machi 30, mwaka huu, lakini akaendelea na kazi.
Kwa bahati mbaya, katika mchezo wa kwanza na Rabat, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Atudo alitonesha bega hilo na kushindwa kuendelea na mechi dakika ya saba tu akimpisha Luckson Kakolaki.
Kwa sababu hiyo, kocha Muingereza Stewart Hall aliamua Atudo akae nje na asiguse kabisa mpira hadi timu itakapofika Morocco, ili kulipa mapumziko bega hilo lipone sawa sawa- shukrani limepona sasa.
Kwa kupumzishwa Atudo, Stewart alikosa mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe Azam FC, Desemba mwaka jana katika dirisha dogo, nafasi yake akicheza Aggrey Morris Ambroce katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union Ijumaa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Ijumaa iliyopita Azam ikitoa sare ya 1-1 na kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa.
Atudo amefanya mazoezi vizuri kwa siku tatu tangu juzi na anaonekana yuko fiti kabisa.
Azam iliwasili hapa Jumatatu baada ya safari ndefu ya takriban saa 14 angani na saa mbili na ushei barabarani- saa tano kutoka Dar es Salaam hadi Dubai na saa tisa kutoka Dubai hadi Cassablanca- kisha saa mbili kwa barabara hadi Rabat.  
Iliondoka Dar es Salaam Jumapili saa 11:00 jioni na kufika Dubai saa 6:00 ambako ililala hadi asubuhi ya jana ilipoondoka kuja Morocco na wachezaji walifika wamechoka kwa uchovu wa safari ndefu.
Ikumbukwe, Azam inayoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Afrika, inahitaji sare yoyote ya mabao au kushinda, ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa Dar es Salaa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdallah hapa Rabat, wenye uwezo wa kukusanya mashabiki 52,000 kuanzia saa 11:00 kwa saa za hapa, sawa na saa 1:00 kwa saa za nyumbani, Tanzania.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video