Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
27 wa Atletico Madrid amekuwa gumzo kuelekea dirisha la usajili,
akiwaniwa na klabu kadhaa zikiwemo Chelsea na Manchester City pia.
Lakini mshambuliaji wa zamani wa
Newcastle, Asprilla anaamini nyota huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni
46 anaweza kutua Old Trafford msimu ujao.
Atapendezaje? Fikiria vipi Radamel Falcao ataonekana katika jezi ya Manchester United
Anawaniwa: Radamel Falcao
Asprilla amesema: "Tulizungumza na
aliniuliza mimi maoni yangu aende timu gani. Anafahamu kwamba kila klabu
kubwa duniani inamtaka. NI mchezaji asiyehadaika na fedha - anachotaka
ni sehemu ambayo familia yake itafurahia na ambako atapata mafanikio.
"Na timu kama Real Madrid, PSG,
Manchester City zina wakati mzuri kuliko zinavyokuwa na wakati mbaya -
na ndiyo maana nikamuambia lazima achague Manchester United. Kila msimu
wanapigana - na ikiwa anataka mafanikio huko ndiko ambako nimemuambia
aende.
Asprilla anaamini Falcao atakuwa
mchezaji pekee daima kucheza Ligi Kuu ya England ambaye anaweza kufanya
vitu kama Alan Shearer.
"Ni vigumu kwangu kufafanua ni mzuri
kiasi gani - ni mmaliziaji mzuri zaidi duniani. Mchezaji pekee
aliyecheza Ligi Kuu England ambaye ana kiwango chake cha umaliziaji ni
Alan Shearer.
"Ikiwa atasaini Manchester United -
atawasaidia kupata taji la Ligi ya Mabingwa. Robin van Persie na Radamel
watakuwa hawakamatiki,".
Muuwaji: Falcao amekuwa hakamatiki anapokuwa mbele ya mdomo wa lango Atletico Madrid
0 comments:
Post a Comment