Na Baraka Mpenja kwa Sportsmail.com
Washika
bunduki wa jiji la London chini ya kocha Mfaransa Mzee Arsene Wenger
wanapanga kuvunja benki ili kumsajili nyota wa Manchester United Wayne
Rooney ili kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya kuondokewa na
aliyekuwa nahodha wao Robin Van Persie aliyejiunga na United.
Mtandao wa Sportmail
amebaini kuwa Arsenal wameonesha utayari wa kumnasa Rooney ambaye msimu
wa ligi England uliomalizika mei 19 hakuwa na mahusiano mazuri na kocha
wake kibabu Alexndar Chapman Ferguson aliyestaafu kuifundisha united na
mikoba yake kukabidhiwa kwa aliyekuwa kocha wa Everton David Moyes.
Endapo
Rooney atakubali kumwaga wino kwa wakali hao wa London kaskazini,
atalipwa msharahara wa pauni laki mbili na nusu kwa wiki.
Nyota
huyo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na United, kitita
ambacho Arsenal wanatarajia kumlipa inasemekana kinaweza kumvutia na
kumwaga wino Emirates.

Wayne Rooney anasemekana anataka kuihama United
Endapo Rooney atasaini mktaba na Arsenal kwa mshahara unaotajwa basi atakuwa mchezaji ghali zaidi katika klabu ya Arsenal.
Nyota
wa Arsenal Lukas Podolski na Theo Walcott kwa sasa ni wachezaji
wanaolipwa kiasi cha pauni laki mbili kwa wiki, lakini kama Rooney
atasaini atalipwa pauni milioni laki mbili na nusu.

Rooney amepata wakati mgumu sana baada ya RVP kujiunga na United akitokea Arsenal


Anataka kuimarisha kikosi: Kocha wa Arsene Wenger anatafuta wachezaji kwa kuimarisha kikosi chake
0 comments:
Post a Comment