Na Baraka Mpenja Kwa msaada wa Sportsmail.com
Walikuwa
wote Chelsea mwenzake kafukuzwa, kapewa timu akiwa meneja mkuu
katimuliwa na Abramovich, sasa mwenzake Mourinho anakuja kuchukua mikoba
ya Rafa Benitez, yeye ni kocha wa Spurs.
Haitoshi
leo hii imempa shavu kubwa mreno mwenzake na sifa nyingi, anataka
nayeye arejee darajani akiwa msaidizi wa msema ovyo au vipi?.
Kocha
wa Tottenham Hospur na aliyefukuzwa kazi na mmiliki wa klabu ya Chelsea
ya London, Roman Abramovich, Mreno Andre Villas-Boas amesema klabu yake
hiyo ya zamani itanyakua ubingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza
chini ya kocha Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho anayeifundisha Real
De Madridi kwa kwasasa, lakini anasemekana kukubali kurudi England
tangu aondoke 2006 darajani.
Villas-Boas
aliyefanya kazi na Mourinho akiwa Chelsea na Inter Milani anaamini
Mreno mwenzake mara atakaporejea darajani ataibadilisha timu ya Chelsea
na kuwa kisima cha burudani na ushindi kwa mashabiki wake.
AVB
aliongeza kuwa Mourinho atabadili umiliki wa timu za jijini Manchester,
yaani Manchester united na Manchester City ambazo zinashindana zaidi
kutafuta ubingwa wa England kuliko timu za London, Chelsea, Arsenal,
Tottenham na Arsenali.
AVB
alisema, “Nafikiri Chelsea itakuwa timu ya kuzifunga timu nyingi msimu
ujao, Mourinho atakuja kuijenga timu bora zaidi na itaipa nafasi ya kuwa
na kikosi bora hivyo watashinda taji la ligi kuu”.
“Lakini
mwaka ujao utakuwa mwaka mzuri kwa Chelsea kama viongozi wa juu ataamua
kufanya maamuzi mazito ya kumchukua kocha huyo mwenye sifa nyingi”.
Aliongeza AVB.
Akizungumzia
timu yake ya Spurs, AVB alisema hajui nini kitatokea msimu huu, lakini
viongozi wa klabu hiyo wajue kuwa wanahitaji kuboresha kikosi kwa
kusajili wachezaji wazuri zaidi ili kuzipa changamoto timu za juu.
“Nafikiri
kama nikiifikisha timu nafasi ya nne itakuwa nzuri zaidi na nitakuwa
nimefikisha mahitaji ya klabu yangu ambayo ni kucheza ligi ya mabingwa
barani ulaya”. Alisema Villas-Boas.

Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas (kushoto) anasema Chelsea atatwaa ubingwa msimu ujao



MARAFIKI
WA ZAMANI WA MOURINHO: Villas-Boas (katikati kushoto) na Jose Mourinho
(wapili kutoka kushoto) walipokuwa Chelsea pamoja
0 comments:
Post a Comment