Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo , wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo(katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo akikazija jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye halfa ya uzinduzi wa program ya Airtel 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Kaimu katibu mkuu wa TFF Kayuni Baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012 wakisalimiana na Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo Wakizindua program ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012
Dar es Salaam, Jumanne 28 Mei 2013…
Airtel
Tanzania leo imezindua michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Airtel imesisitiza dhamira yake ya
kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na serikali kukuza
vipaji vya soka nchini Tanzania.
Huu
ni mwaka wa tatu mfululizo tangu kampuni ya airtel ianze kudhamini
mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo huanzia ngazi ya mkoa hadi
Taifa. Fainali za Airtel Rising Stars Taifa hufatiwa na kliniki ya soka
ya kimataifa kwa wachezaji nyota chini ya ukufunzi wa makocha mahili wa
vijana kutoka klabu ya Manchester United.
“Nafurahi
kwamba tumepiga hatua na leo tunazindua msimu wa tatu wa Airtel Rising
Stars ambao bila shaka utakuwa wa ushindani na wa kusisimua”, alisema
Beatrice Singano, Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya Airtel Tanzania.
Uzindinduzi huo ulifanyika katika ofisi za TFF.
Singano
alisema: “Airtel imevutiwa na mwitikio wa vijana wengi waliojitokeza
kujiandisha na kushiriki katika mashindano ya Airtel Rising Stars katika
miaka iliyopita. Ni matumaini yetu kwamba vijana wengi zaidi
watajitokeza kushiriki mwaka huu”.
Singano
alisema mpango huu kabambe unawalenga wasichana na wavulana nchi nzima
ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa mawakala wa soka, makocha
na mamlaka nyingine zinazohusika na programu za kuendeleza vipaji vya
soka. Mwaka huu Airtel Rising Stars itajumuisha jumla ya timu 24 za
wasichana na wavulana kutoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Morogoro, Ilala, Kinondoni Temeke, Kigoma, Tanga na Ruvuma
ambao baadhi yao watateuliwa kuunda timu za mikoa yao katika fainali za
Taifa. Vile vile mashindano ya Taifa yatatumika kuteua timu
itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa (inter-country
tournament)
Akizunguma
katika hafla hiyo, mgeni rasmi Mkurugezi wa Michezo nchini Bw. Leonard
Thadeo alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na Airtel kuwekeza
kwenye programu ya soka ya vijana ambao ndiyo nguzo mhimu kwa maendeleo
ya mchezo wa soka nchini. Kauli yake iliungwa mkono na Makamu wa Pili
wa Rais wa TFF Bw Basibu Ramadhani ambaye alisema program za soka za
vijana ndio njia pekee ya kuinua kiwango cha soka nchini.
“Tumeshudia
vipaji vingi katika mashindano yaliyopita na bila shaka michuano ya
mwaka huu yataendelea kutoa vipaji vingine vingi. Natowa wito kwa timu
kubwa hapa nchini kutumia fursa hii kupata wachezaji chipukizi kwa ajili
kuimarisha timu zao. Nawatakia washiriki wote mashindano mema na
wazingatie nidhamu na taratibu ya mchezo wa soka.” alisema Thadeo.
Programu
hii ya Afrika inaungwa mkono na klabu kubwa ya Manchester United kwa
lengo la kubaini vipaji vya soka na kuviendeleza ili kuweza kuonekana
kwa mawakala, makocha na kupata nafasi ya kutambulika kitaifa na
kimataifa.
Ushirikiano
wa Airtel na Manchester United katika kuendeleza soka ya vijana ni
utekelizaji wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili
mwezi Disemba 2010 ambayo yanaiwezesha Airtel kutumia hazina ya ufundi
wa soka kutoka klabu hiyo kubwa duniani kuendeleza vijana chipukizi
barani Afrika.
Vijana
wanaoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu hapa nchini wanatajiwa
kuanza kujiandikisha mwezi ujao na jumla ya timu 24 kutoka mikoa 9
zitashiriki.
Airtel
ni kampuni ya simu za mikononi inayofanya biashara barani Afrika katika
nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Democratic Republic of
Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda,
Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia.
0 comments:
Post a Comment