Na Baraka Mpenja
Baada
ya kuporomoka daraja msimu wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika
mei 18 mwaka huu, maafande wa Polisi Morogoro wamesema wamewapa
mapumziko ya wiki mbili wachezaji wao na baada ya hapo watarudi kambini
kuweka mikakati ya kurudi ligi kuu msimu wa 2014/2015.
Afisa habari wa klabu hiyo Clemence Banzo ameimbia MATUKIO DUNAINI
Kuwa wameamua kuwabakisha wachezaji wao wote ili kuhakikisha ndani ya
mwaka mmoja wanarudi ligi kuu na kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki
wa kandanda mjini Morogoro.
“Kushuka
daraja haikuwa mipango yetu, tulikosa sapoti kutoka kwa wadau na
viongozi wa jeshi kitaifa, lakini kama tutabahatika kurudi ligi kuu,
hakika tutazungumza na viongozi wetu wa wizara ili waisaidie timu moja
ya polisi kupata msaada” .Alisema Banzo.
Akizungumzia
ushindani wa timu za majeshi michuano ya ligi, Banzo alisema timu hizo
zinajitahidi sana ingawa kuna changamoto za kifedha.
Banzo
alisema baadhi ya timu hizo zinasaidiwa sana huku akitolea mfano klabu
ya Tanzania Prisons ambayo hupewa msaada kila mkoa inapoenda kucheza
mechi.
Afisa
habari huyo aliongeza kuwa kwa sasa kuna haja kwa jeshi la Polisi
Tanzania kutengeneza timu nzuri ya kuliwakilisha jeshi hilo kitaifa na
kimataifa kama nchi nyingine.
“Tunakosa
misaada sana kwa kweli, imekuwa ngumu sana kuendesha klabu yetu, kama
sio wadau wa soka mkoani Morogoro tungekuwa na hali ngumu sana, lakini
tanajipanga vizuri kurejea ligi kuu bara”. Aliongea Banzo kwa kujiamini.
Kuhusu
kocha wao Rishard Adolf, Banzo alisema wapo katika mazungumzo na kocha
huyo ili aendelea kuifundisha klabu yake na airudishe ligi kuu kwa mara
nyingine.
“Adolf
ametusaidia sana na ndio maana baada ya kuchukua timu msimu wa pili
alifanya vizuri sana, alijenga morali ya wachezaji na kupata matokeo
mazuri, tunadhani hakuna haja ya kumuachia kocha huyo mwenye uezo
mkubwa”. Alisema Banzo.
0 comments:
Post a Comment