Kiungo huyo wa Ivory Coast mwenye umri
wa miaka 29, amekubali mkataba mpya wenye thamani ya Pauni Milioni 11
kwa mwaka, wiki kadhaa baada ya kuripotiwa anataka kuondoka klabu hyo.
Mshahara wake wa zaidi ya Pauni 210,000 kwa wiki utabaki vile vile.

Mambo yamekuwa mambo! Yaya Toure
akizungumza na simu huko Carrington leo baada ya kukubali mkataba mpya
wa miaka minne Manchester City wenye thamani ya Pauni Milioni 45.
Toure, ambaye alijiunga na klabu hiyo
akitokea Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 24 majira ya kiangazi mwaka
2010, alionekana kupagawa awali na kusuasua kwa majadiliano ya mkataba
mpya na wakala wake, Dimitri Seluk akakaririwa akisema kiungo huyo
anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu.
Lakini mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu wamemalizana haraka na mkali huyo na leo watatangaza rasmi mkataba wake mpya.

Kifaa: Toure amekuwa tegemeo kubwa katika safu ya kiungo ya Man City tangu awasili akitokea Barcelona mwaka 2010
0 comments:
Post a Comment