Mabingwa wa ligi ya Bundesliga ya nchini ujerumani, The Bavarian Bayern Munich wameanza vyema kampeni ya kuelekea kucheza fainali ya tatu ya Ligi ya Mabingwa barabi Ulaya ndani ya miaka minne, baada ya kuwazamisha bila huruma wale wanaodaiwa kuwa bora zaidi kuwahi kutoka katika hii dunia, Wakatalunya FC Barcelona mabao 4-0 usiku huu kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya kwanza.
Mabao
mawili kutoka kwa Thomas Muller na moja kwa kila mmoja, Mario Gomez na
Arjen Robben yamempa faraja kocha Jupp Heynckes ambaye sasa sijui itokee
miujiza gani Jumatano ijayo Uwanja Nou Camp kwenye mchezo wa marudiano
akose tiketi ya kwenda Wembley.
Katika
mchezo huo wa kukata na shoka na uliovuta hisia za mamilioni ya
mashabiki wa soka duniani ulianza kwa vijana wa Munich kucheza soka la
kasi na nguvu kama ilivyokwaida yao.
Bayern
walionesha kuwa na morali kubwa zaidi ya kuhitaji matokeo ya ushindi
mbele ya “Catalan Boys” wanaosifika kwa soka la pasi fupi fupi za na za
uhakika zaidi.
Kipigo
cha jana ni adimu sana kwa Barca kwa siku za karibuni lakini jana
hawakuwa na jinsi kutokana na uwezo mkubwa wa wapinzania wao.
Labda miijuza ya soka isubiriwe huko Hispania kama wataweza kupindua kipigo hicho kwa misumari minne kwa ubuyu.
Wakati
Bayern wakingara zaidi Allianz Arena, Nyota wa Barca Lionel Andrew
Jorge Messi alibanwa mpaka alitia huruma katika mchezo huo.
Kikosi
cha Bayern Munich kilichofanya mauaji hayo kilikuwa: Neuer, Lahm,
Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Robben,
Muller/Pizarro dk83, Ribery/Shaqiri dk88 na Gomez/Gustavo dk71.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro/Villa dk83.

Fundi mwenye shabaha na akili ya kandanda Thomas Mueller akishangilia baada ya kutia kimiani bao la kwanza

Fainali
hiyooooo!: Nyota wa Bayern Munich, supa Mario Gomez na mchezaji
mwenzake, mtaalamu Javi Martinez wakishangilia baada ya kupata bao la
pili

Winga machachari na mwenye kasi kama mshale Mholanzi Ajen Robben akishangilia mbele ya mashabiki baada ya kufunga bao lake

Huruma:
Mwanasoka bora wa dunia mara nne mfulullizo wa FIFA raia wa Argentina
na mshambuliaji wa Barca, Lionel Andrew Jorge Messi akionekana aliyekata
tamaa

Messi
na Barcelona wanakabiliwa na mchezo mgumu wa marudiano kutokana na
ubora walionao The Bavarian Bayern Munich mabingwa wa Bundes Liga
LEO KIVUMBI KINGINE
Leo
nusu fainali nyingine inasubiriwa baina ya miamba ya sola nchini
Hispani, Real De Madrid chini ya kocha maarufu duniani, Mreno Mario Jose
Dos Santos Ferlix Mourinho dhidi ya nyuki wa kaskazini mashariki mwa
Ujerumani na wenye machungu ya kupoteza ubingwa wao, Borrusia Dortmund.
Mechi hiyo itapigwa nchini Ujerumani na wiki ijayo Santiago Bernabeu.
0 comments:
Post a Comment