WAREMBO wenye sifa za kushiriki shindano la Redds Miss Tanga, wametakiwa kujitokeza kushiriki shindano katika kuwania taji la Miss.
Akizungumza na Vyombo vya Habari
Mkurugezi wa Kampuni ya datk Intertaimeint, Asha Kigundula alisema kwa
maandalizi ya shindano hilo ndiyo yanaanza na kutaka warembo wajitokeza
kushiriki.
Asha alisema fomu zitapatikana
katika ofisi ya Mwananchi iliyopo bandari Tanga gorofa ya Nne, Five
brathers kwa nassa makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam
zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo jingo la Hifadhi Hause
Posta.
“Mazoezi kwa warembo yataanza
ijumaa ya Mei 3 mwaka huu jijini Tanga, warembo hao watakuwa chini ya
walimu wawili ikiwa ni pamoja na mshindi wa mwaka jana wa mkoa huo
Teresia Kimolo”alisema Asha.
Alisema kwamba shindano la mwaka
huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni datk
imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa
ujumla wakae mkao wa kupata raha.
0 comments:
Post a Comment