Kikosi cha wana TamTam wakipiga wakipiga dua kwa mungu wao
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Nyota
wa watengeneza sukari wa mashamba ya miwa Manungu Turiani mkoani
Morogoro, klabu ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu amerejea kikosini na
kuendelea na mazoezi ya kocha mkuu wa timu hiyo, nahodha wa heshima wa
taifa stars, Merck Mexme kwa ajili ya mtanange wa ligi kuu soka Tanzania
bara mei mosi mwaka huu dhidi ya vibonde Africa Lyon dimba la Manungu
Complex.
Javu
ambaye timu nyingi zinamkodolea jicho la tatu ili kuinasa saini yake
msimu ujao, alikuwa anasumbuliwa na majeruhi ya hapa na pale lakini
sasa yuko shwari na anapiga jalamba kama kawaida maeneo ya Manungu
Turiani.
Akizungumza kwa njia ya simu na MICHEZO BOMBA!
kutoka Manungu, Meneja wa wana TamTam hao, David Bugoya alisema kwa
sasa kikosi kipo salama na kinaendelea na mazoezi huku habari njema kwa
mashabiki wa klabu hiyo ni urejeo wa mshambuliaji Nguli Hussein Javu.
“Tunamshukuru
Mungu tunaendelea vizuri na mazoezi yetu hapa Manungu, vijana wana
morali kubwa ambayo inachagizwa na ushindi wa 1-0 mechi iliyopita dhidi
ya Oljoro, pia Javu yupo fiti kuwakabili Lyon mei mosi hapa Manungu”.
Alisema Bugoya.
Javu
ni miongoni wa washambuliaji walioitwa na Kocha mkuu wa timu ya taifa ya
Tanzania “Taifa stars” Mdenish Kim Paulsen ili kuunda kikosi cha Young
Taifa stars ambacho kimejumuisha wachezaji vijana na wakubwa ambao
hawajapata nafasi ya kucheza timu ya kwanza.
Bugoya
aliongeza kuwa mipango yao ni kupata ushindi mnono nyumbani kutokana na
mazoezi ya uhakika wanayoyafanya Manungu, lakini alisisitiza kuwa soka
lina matokeo ya aina yake hivyo ikiwa tofauti na mipango yao itabidi
wakubali hali hiyo.
Afrca
Lyon wakiwa chini ya kocha wake Mkenya Charles Otieno jahazi lao
linakwenda mrama msimu huu na kuna uwezekano mkubwa wa kushuka daraja
kutokana na kuburuza mkia mpaka sasa wakijikusanyia pointi 19 tu.
Mtibwa
wapo nafasi ya tano wakijikusanyia pointi 36 na kama watashinda mchezo
huo watazidi kujijengea nafasi nzuri ya kusaka nafasi tatu za juu ambapo
mapambano ni baina ya klabu za Coastal Union “wagosi wa kaya”, Wana
“Nkulukumbi” Kagera Sugar, Simba na Azam Fc “wana lambalamba”.
0 comments:
Post a Comment