Na Baraka Mpenja
Wakati
Watanzania wakiadhimisha miaka 49 ya Muungano, kwa wale wapenda
kandanda watakuwa wanafuatilia mechi ya kukata na shoka baina ya Wagosi
wa Kaya wanaonolewa na kocha Hemed Morroco dhidi ya wana lambalamba
kutoka Chamazi Klabu ya Azam fc dimba la Chama cha Mapinduzi Mkwakwani
jijini Tanga “Waja leo waondoka” leo.
Mchezo
wa leo ni mgumu sana kwa timu zote kutokana na uhitaji mkubwa wa mzigo
wa pointi tatu kwa timu zote ili kujiweka mazingira mazuri katika
msimamo wa ligi ambapo Azam wanawania ubingwa na Coastal wanahitaji
nafasi ya pili.
Endapo
wana lambalamba watashinda leo watafikisha poinbti 50 nyuma ya Yanga
wenye pointi 56 kileleni na wakihitaji pointi moja tu katika michezo
miwili iliyosalia ili kujitangazia ubingwa msimu huu wa 2012/2013.
Kila
kukicha Azam wanamwombea dua mbaya Yanga ili apoteze michezo miwili
ijayo dhidi ya Coastal Unioni na Mnyama Simba hivyo kuwa na matumaini ya
kupata ubingwa wao wa kwanza tangu waanze kushiriki michuano ya ligi
kuu soka Tanzania bara msimu wa 2007/2008.
Wawakilishi
hao pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa wanapigana kufa na
kupona ili kuweka historia ya kutwaa ndoo yaligi kuu ambayo mabingwa
watetezi Simba wapo chali na wamekubali kuupoteza.
Wakati
huo huo Viongozi saba wa klabu ya Azam fc wakiongozwa na katibu mkuu wa
klabu hiyo Alhaji Idrisa Nassor wanakwenda nchini Morroco leo kwa lengo
la kufanya maandalizi ya mwanzo kabla ya timu yao kusafiri jumanne ya
wiki ijayo.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga alisema wanaondoa leo kwa ndege
ya Emirates saa 11 jioni uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es
salaam.
“Hata
viongozi wa serikali wanaposafiri kwenda sehemu Fulani kufanya ziara
wanatuma watu kwa sababu za usalama, sisi pia kwa kufuata utamaduni huo
lazima baadhi yetu tuwahi kule kuangalia nini kinachoendelea huko ”.
Alisema Idd.
Idd aliongeza kuwa kila wanapoenda ugenini lazima watangulize viongozi na baadaye timu inapokelewa nao.
Afisa
habari huyo aliwataka watanzania kuwaombea dua njema kwani
hawatawaangusha hata kidogo kutokana na uwezo wa timu yao na maandalizi
kwa ujumla.
“Walikuja
hapa AS FAR Rabat tukatoa nao suluhu, siyo mbaya sana kwetu, tunahitaji
ushindi wowote , kama tutapata bao moja la ugenini, tutawachanganya
zaidi wapinzani wetu, tuombeane watanzania wote”. Alisema Idd.
0 comments:
Post a Comment