Kikosi cha Kagera Sugar katika moja ya mechi za nyuma za ligi kuu Tanzania bara
Na Baraka Mpenja
Watengeneza
sukari wa kaitaba mkoani Kagera, klabu ya Kagera Sugar tayari
imeshawasili mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wao wa jumatano ya wiki
hii uwanja wa Jamhuri dhidi ya maafande wa Polisi Morogoro ambao jana
wametandikwa bao 2-1 na Mnyama Simba na kuzidi kupoteza matumaini ya
kusalia ligi kuu bara msimu huu.
Akizungumza na MICHEZO BOMBA! kocha
mkuu wa wana “Nkulukumbi” Kagera Sugar Abdallah King Kibadeni “Mputa”
alisema timu imewasili usiku wa jana na leo wanatarajia kufanya mazoezi
katika uwanja wa Jamhuri.
“Timu
iko salama, tunajiandaa kupambana na Polisi Morogoro ambao wanahitaji
ushindi kwa vyoyote vile hususani baada ya kufungwa jana na Simba,
tunatambua watapigana kufa na kupona lakini tuko shwari”. Alisema
Kibadeni Kutokea mkoani Morogoro.
Kibadeni
mwenye ndoto za kushika nafasi ya pili msimu huu alisema kuwa kabla ya
kusafiri kwenda Mji kasoro bahari walipitia mkoani Gieta ambapo
walicheza mechi mbili za kirafiki ili kupima ubavu kikosi chao.
“Tumetokea
Gieta, tumecheza mechi mbili, moja ilikuwa dhidi ya kikosi cha vijana
chini ya miaka 20 wa mkoani Geita na tukawafunga mabao 2-0 na ya pili
tulicheza na wachimba madini wa Mgusi FC na kuwafunga mabao 2-1, mechi
hizi zimenisaidia kutambua makosa ya wachezaji wangu”. Alisema Kibadeni.
Kagera
sugar inajiandaa kupambana na Polisi Moro ambayo ipo nafasi ya pili
kutoka mkiani akijikusanyia pointi 19 baada ya kutandikwa na simba
mabao2-1 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jana.
Kwa
mujibu wa Viongozi wa Polisi Moro, tayari wameshakiri kuwa wana
uwezekano mkubwa wa kutoa mkono wa bai bai kwa michuano ya ligi kuu
Tanzania bara msimu huu.
0 comments:
Post a Comment