Timu
za Coastal Union ya Tanga na Azam zitapambana Aprili 26 mwaka huu katika
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) itakayofanyika kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Awali
mechi hiyo namba 168 ilikuwa ichezwe Aprili 27 mwaka huu, lakini
imerudishwa nyuma kwa siku moja ili kuipa fursa Azam kujiandaa kwa mechi
ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR
Rabat ya Morocco.
Mechi
hiyo itachezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani akisaidiwa na
Abdallah Mkomwa (Pwani), Vicent Mlabu (Morogoro) wakati mwamuzi wa
mezani atakuwa Mohamed Mkono wa Tanga. Charles Komba wa Dodoma ndiye
atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya 24.
Baada
ya mechi ya Tanga, Azam itarejea Dar es Salaam siku inayofuata tayari
kwa safari ya kwenda Rabat itakayofanyika Aprili 28 mwaka huu. Mechi
hiyo itachezwa wikiendi ya Mei 3, 4 au 5 mwaka huu.
Keshokutwa
(Aprili 24 mwaka huu) kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
African Lyon na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es
Salaam.
Iwapo
Azam itafanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho
kutakuwa na marekebisho ya ratiba ya VPL. Hiyo ni kutokana na raundi
inayofuata ya Kombe la Shrikisho kuchezwa wikiendi ya Mei 17, 18 na 19
mwaka huu ambapo bado haijajulikana Azam itaanzia wapi (nyumbani au
ugenini) iwapo itavuka.
Mechi
nyingine za VPL mwezi ni Aprili 25 (Ruvu Shooting vs Simba- Uwanja wa
Taifa), na Aprili 28 (Simba vs Polisi Morogoro- Uwanja wa Taifa).
0 comments:
Post a Comment