Na Baraka Mpenja
Vuvuzela
mpya zitakazotumiwa na mashabiki wa fainali za kombe dunia mwakani
nchini Brazil ambazo zinasemekana kutokuwa na kelele za kuwakera
mashabiki kama zile zilitumiwa nchini Africa Kusini 2010 zimeshapatikana
na zina ubora mkubwa kuliko za mwanzo.
Vuvuzela
hiyo inaitwa Caxirola itakuwa ya plastiki kama za Africa kusini lakini
haitaweza kuwakera wachezaji wanapokuwa uwanjani.
Tofauti
na Vuvuzela ambazo ni tamaduni za watu wa Afrika kusini, Vuvuzela mpya
zilizobuniwa kwa sasa ni maalumu kwa kushangilia soka.
Nao
FIFA wamekubali ubora wa kifaa hicho na kitatumiwa na mashabiki wa soka
ili kuhamisha timu zao kucheza kandanda wakati wa fainali hizo zakombe
la dunia nchini Brazil.

Rais
wa Brazil Dilma Rousseff akiwa ameshika caxirola, Vuvuzela mpya kwa
ajili ya kushangilia fainali za kombe la dunia mwakani.

Mtoto Mdogo raia wa Cameroonian na shabiki wa soka akipuliza Vuvuzela yake katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010.



Rais
wa Brazil Dilma Rousseff, mwanasanaa Carlinhos Brown na waziri wa
utamaduni nchini Brazil Marta Suplicy wakiziangalia Vuvuzela za kuimbia
wimbo wa taifa

Hawa ni mashabiki wa Bafana Bafana walipokuwa wanapiga Vuvuzela kwenye fainali za 2010 nchini mwao
0 comments:
Post a Comment