![]() |
YANGA |
Na Baraka Mpenja
Ligi kuu Tanzania bara kuendelea kesho
kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la taifa lenye nyasi nzuri baina ya
vinara Dar Young Africans dhidi ya wapiga gwaridi wa JKT Ruvu kutoka mkoani
Pwani.
Yanga yenye pointi 53 itashuka uwanjani
kuhitaji pointi tatu muhimu baada ya kubanwa mbavu mchezo uliopita na maafande
wa Mgambo JKT kwa kutoka nao sare ya 1-1 katika uwanja wa CCM Mkwakwani Mkoani
Tanga.
Kuelekea katika mchezo huo wa kesho Yanga
kupitia kwa afisa habar wake Baraka Kizuguto walisema maandalizi yamekamili na
wachezaji wote wapo salama kambini kinachosubiriwa ni muda mwafaka kuwadia.
“Mchezo dhidi ya Mgambo waamuzi
walichezesha madudu, waliwabeba wapinzani wetu na ndio maana tulishindwa kutwaa
pointi tatu, tumerejea uwanja wa nyumbani tukiwa kikosi kamili, JKT Ruvu
wataoneshwa soka safi na la kuvutia”. Alisema Kizuguto.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa
wanawashukuru mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti kubwa na amewaomba
kujitokeza kwa wingi uwanja wa taifa hapo kesho kuwashangilia ili waibuke
kidedea.
JKT Ruvu wanahitaji ushindi ili kuendelea
na harakati zao za kujinusuru kushuka daraja msimu huu.
Kesho kivutio kwa mashabiki wa soka ni kumwona
tena nyota wa zamani wa simba ambaye ana historia ya kuwafunga Yanga, Musa
Hassan Mgosi ambaye sasa anakipiga katika klabu ya JKT Ruvu.
Mgosi kesho uatajaribu kuwafung Vinara yanga
akiwa na timu tofauti na wapinzani wa karibu wa Yanga.
Mbali ya
mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa mwezi huu ni kati ya African Lyon na JKT
Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati
Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Nayo
Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika
mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja wa Taifa utakuwa mwenyeji wa mechi kati
ya Simba na Polisi Morogoro itakayofanyika Aprili 28.
0 comments:
Post a Comment