Na Baraka Mpenja wa fullshangwe Dar
es Salaam.
Baada ya mapumziko wa sikuu ya Pasaka,
vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Dar Young Africans maarufu kama
“Wazee wa Uturuki” kesho wanaingia kambini kujiandaa na mchezo ujao wa aprili
10 mwaka huu dhidi ya wapiga gwaride wa JKT Oljoro dimba maridhawa la taifa
chang`ombe jijini Dar es Salaam.
Akiongea Kwa tambo nyingi, afisa
habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, amesema hakuna wa kutwaa taji la ligi kuu
msimu huu zaidi ya Yanga wenye pointi 49 kileleni wakifuatia na wawakilishi
pekee wa Tanzania mashindano ya kimataifa, wana lambalamba Azam fc waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi
43.
“Kesho tunaanza mawindo yetu dhidi ya
Oljoro, kikubwa mashabiki wetu waje kwa
wingi siku ya mechi kama walivyofanya Morogoro kwani vijana wao wenye uchu wa
kutwaa mwari msimu huu hawatawaangusha siku hiyo”. Alitamba Kizuguto.
Kizuguto alisema walifanya mikakati
mikubwa ikiwa ni pamoja na kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki ili
kuwapa nguvu wachezaji na sasa wanavuna mavuno ya kambi hiyo bora nchini humo.
“Mashabiki wa Yanga wasiwe na
wasiwasi, tumejipanga sana, cha muhimu tunaongoza ligi na hakuna wa kutufikia
kwa poniti zetu 49, tushikamane ili tupate mafanikio tuliotarajia”. Alisema Kizuguto.
Afisa habari huyo wa watoto wa mitaa
ya Twiga na Jangwani aliongeza kuwa licha ya kuwa na uhakika wa kutwaa kombe
msimu huu, wanadhamiria kufanya vizuri mechi zote zilizosalia ili kulinda
heshima yao.
Kizuguto alisema mashabiki na
wanachama wa klabu hiyo waendelee kushikama na kuwaombea dua wachezaji wao ili
wawe na afya njema katika mchezo wao na Oljoro.
Pia amesema mpaka sasa hakuna
mchezaji yeyote aliyeripotiwa kuwa majeruhi, lakini kesho watatoa taarifa baada
ya kukutana na wachezaji wote mazoezini.
Jumamosi wiki iliyopita Vinara Yanga
waliambulia pointi moja katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro baada ya
kubanwa mbavu na vijana wa Rishad Adolf, maafande wa kupiga kwata, Polisi
Morogoro , mchezo uliomalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.
0 comments:
Post a Comment