
Na Baraka Mpenja, Dar
es Salaam
Burudani kubwa kwa wapenzi wa
masumbwi inatarajiwa kufanyika aprili saba mwaka huu ukumbi wa CCM Mwinjuma ,
Mwananyamala jijini, Dar es salaam, ambapo bondia Issa Omary na Shaban Madilu
watapanda ulingoni katika pambano la raundi 10 kuwania ubingwa wa UBO (Universal boxing organization International)
.
Katibu mkuu wa oganizesheni ya ngumi
za kulipwa Tanzania (TPBO) na mratibu mkuu wa pambano hilo, Ibrahim Kamwe `Big
Light` amesema pambano hilo linatarajia kuwa la kukata na shoka kutokana na
ubora wa mabondio wote wawili.
“kama unapenda masumbwi hakika ni
siku nzuri kwako kuona ulingo ukihimili mikikimikiki ya mabondia ambao
wamekamiana sana kutokana na upinzani wao wa muda mrefu, nawaomba watu wafike
kwa wingi”. Alisema Kamwe.
Akizungumzia kiingilio cha kuona
burudani hiyo, Kamwe alisema kuwa
wameamua kuweka kiingilio cha kawaida cha shilingi elfu nne (4,000/=) za
kitanzania kutokana na watu wengi kutoka katika msimu wa sikuu ya pasaka.
Kamwe aliongeza kuwa siku hiyo
mapambano yataanza majira ya saa kumi jioni, hivyo ni muhimu kwa wapenzi wa
masumbwi ama ndonnga kuwahi kufika ukumbini ili kupata burudani maridhawa.
Mratibu huyo alisitiza kuwa siku hiyo
yatakuwepo mapamabo mengi ya utangulizi kabla ya wanaume wawili watakaowania
ubingwa kupanda ulingoni kuoneshana umwamba mbele ya umati wa mashabiki
watakaofurika ukumbini hapo.
“Ili kuhakikisha buruadani inakuwa
nzuri, tumeandaa mapambano ya utangulizi, Bondia Ramadhan Kido atapanda
ulingoni na Musa Mbabe,Joseph Marwa ataoneshana ubaunsa na Amour Mzungu wakatai
huo huo Mwaite Juma atatunishana msuli na Hussein Mbonde, hakika usikose siku
hiyo”. Alisisitiza Kamwe.
Akizungumzia hali ya mchezo wa
masumbwi nchini, Kamwe alisema mchezo huo unazidi kujipatia umaarufu , hivyo ni
nafasi kwa wadau kutupia jicho la tatu na kuwekeza kama wanavyofanya kwenye
mchezo wa kandanda.
Kamwe aliongeza kuwa masumbwi yanaweza
kulibeba taifa medani ya kimataifa, hivyo serikali, taasisi za wtu binafsi,
makampuni mbalimbali yanatakiwa kuwekeza katika mchezo huo wenye umaarufu
mkubwa duniani.
0 comments:
Post a Comment