>>BADO YUPO UCHUNGUZI FIFA TUKIO LAKE KUPIGA NGUMI URUGUAY v CHILE!!
>> GRAEME SOUNESS ASEMA HASTAHILI KUCHEZA ANFIELD!!
>>PATA VIMBWANGA 10 VYA SUAREZ!!

Brendan Rodgers ameahidi kupitia Mkanda
wa Video wa tukio hilo na kutoa tamko lakini Meneja wa zamani wa
Liverpool, Graeme Souness, amelaani vikali tukio hilo na kusema umefika
wakati wa Mchezaji huyo kutoka Uruguay kuondolewa Liverpool.
Souness ameng’ang’ania kuwa Liverpool ni
Klabu kubwa yenye hadhi kama Barcelona, Real Madrid a Manchester
United, na Mchezaji huyo anatia dosari sifa ya Klabu.
Tukio hilo la Suarez kumng’ata Ivanovic
lilitokea kwenye Mechi ya BPL, Barclays Premier League, iliochezwa
Anfield na Liverpool kutoka sare 2-2 na Chelsea huku Suarez akishika
makusudi na Chelsea kupata Penati waliyofunga na ni yeye Suarez ndie
alieisawazishia Liverpool katika Dakika za majeruhi.
PATA MATUKIO YA UTATA YA SUAREZ KATIKA ULIMWENGU WA SOKA:
Novemba 2007
Akiwa Nahodha wa Ajax alifungiwa na Klabu yake baada ya kupigana na mwenzake Albert Luque wakati wa Haftaimu kwenye Mechi.
Julai 2010
Afrika na Dunia nzima itamkumbuka
Suarez, ambae ni Mchezaji wa Uruguay, kwa kuikatili Ghana huko Afrika
Kusini kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia alipoushika mpira
kwa makusudi kwenye mstari wa goli dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza
na kuwanyima Ghana goli la wazi la ushindi.
Kwa kitendo hicho, Suarez aliwashwa Kadi
Nyekundu na Ghana kupewa penati lakini Asamoah Gyan, ambae aliwahi kuwa
Ligi Kuu England na Timu ya Sunderland, alikosa kufunga penati hiyo.
Novemba 2010
Alipata Kifungo cha Mechi 7 akiwa huko
Uholanzi na Klabu ya Ajax baada ya kumng’ata meno Mchezaji wa PSV
Eindhoven Otman Bakkal kwenye mechi ya Ligi huko Uholanzi.
Octoba 2011
Wakicheza na Everton, alivunga amechezewa faulo na Jack Rodwell na kujidondosha na Rodwell akapewa Kadi Nyekundu.
Octoba 2011
Suárez alimkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kufungiwa Mechi 7 na kupigwa Faini Pauni 40,000.
Decemba 2011
Akiwa kwenye mashitaka ya kumkashifu
Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kabla hajahukumiwa
alionekana kutoa ishara ya matusi kwa Mashabiki wa Fulham kitendo
ambacho kilimpa Kifungo cha Mechi 1.
Februari 2012
Man United na Liverpool walikutana tena
Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu tukio la Suarez kumkashifu
Kibaguzi Evra na Suarez, bila kutarajiwa, aligoma kumpa mkono Evra.
October 2012
Alishangilia Goli lake kwa kujirusha
mbele ya Meneja wa Everton, David Moyes, ambae kabla ya Mechi hiyo na
Liverpool alitamka Wachezaji wadanganyifu kama Suarez wnaohadaa Marefa
wanafanya Mashabiki waikatae Soka ya England.
Januari 2013
Alipoza mpira kwa mkono na kufunga Bao
la ushindi kwa Liverpool kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP dhidi ya
Timu ya Daraja la chini Mansfield.
Machi 2013
Akiichezea Nchi yake Uruguay kwenye
Mechi ya Mchujo ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil
Mwaka 2014, Suarez alionekana kumtandika ngumi Beki wa Chile Gonzalo
Jara bila Refa kuona.
FIFA wanachunguza tukio hili.
0 comments:
Post a Comment