Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hatimaye
beki wa Chelsea John Terry amewashangaza wengi baada ya kutangaza kuwa
kwa sasa yupo tayari kurudi timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama
“Simba watatu”.
Kwa
mujibu wa gazeti la Sportsmail nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa
ya Uingereza, Terry alijiondoa katika kikosi hicho baada ya chama cha
soka nchini humo FA kumshutumu kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi mwezi
septemba mwaka jana dhidi ya mdogo wake Rio Ferdinand namzungumzia Anton
Ferdinand, lakini sasa amesema yupo tayari kuitwa na kocha Roy Hodgson.
Terry
aliongeza kuwa kwasasa amejiandaa kucheza nafasi ya ulinzi na Rio
Ferdinand endapo wote wataitwa kuunda kikosi cha simba watatu.



Hii
inamaanisha Hodgson ambaye mwaka jana katika fainali za mataifa ya
ulaya alimwacha Ferdinand na kumuita Terry, kwa sasa anaweza kuwaita
nyota hao wawili na wakacheza pamoja safu ya ulinzi dhidi ya Jamhuri ya
Island, mchezo utakaopigwa mei 29 kuwania kufuzu fainali za kombe la
dunia zitakazoanza kutimua vumbi mwezi juni 2014 nchini Brazil.


Terry anajiandaa kucheza na Rio Ferdinand licha kuwepo mgogoro na mdogo wake Rio, Anton Ferdinand (Hapo chini)

Tukio
linginie ambalo Terry alifanya mapema mwezi huu ni kugoma kumsalimia
mwenyekiti wa chama cha soka nchini Uingreza FA, lakini sasa yupo tayari
kurejea timu ya taifa.
Terry alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa baada ya kutuhumiwa kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya Anton Ferdinand


Terry
baada ya kupata tuhuma hizo alifikishwa katika mahakama ya Westminster
Magistrates ambapo mahakama hiyo ilimwachia huru kwa kutokutwa na kesi
ya kujibu wakati FA ilimhukumu kifungo cha kutocheza mechi nne na faini
ya Uro laki mbili na ishirini.
Mechi
ya mwisho kwa Terry kucheza na timu ya taifa ni ile aliyoanzia benchi
dhidi ya Moldova kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwezi septemba
mwaka jana na walishinda bao 5-0.

Terry msimu huu katika klabu yake ya Chelsea mara nyingi amekuwa akisugua benchi

Kocha wa England Hodgson alimjumuisha Terry kikosini badala ya Rio Ferdinand katika fainali za kombe la mataifa ya ulaya.
0 comments:
Post a Comment