Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nyota
wa wekundu wa Anfield Liverpool Luis Suarez amethibitisha kuwa hatakata
rufaa kupinga hukumu yake ya kusimamishwa kucheza mechi 10 kwa kosa la
kumng`ata kwa meno beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, lakini amekiri
kukosea na atabadili tabia nje ya uwanja.
Suarez
amesema, “Kiukweli nawaomba radhi sana kwa kitendo kile, watu wote
niliowaudhi pale Anfield siku hiyo nawaomba wanisamehe sana, lakini
kibinafsi namuomba tena msamaha Ivonovic kwa kitendo kile”.
Nyota
huyo alisema mambo yote yaliyompata huko England yatamsaidia kubadili
tabia yake na kuanzia sasa anataka kujikita kubadili tabia yake na kuwa
mchezaji mzuri uwanjani.

Wakitabasamu:
Suarez alionekana mwenye furaha kubwa katika mazoezi ya leo jioni kabla
ya kuomba msamaha katika mtandao wake wa Twita.
Suarez
aliendelea kueleza kuwa hataki kupotosha ukweli wa kitendo kile kwa
kukata rufaa bali amekubali makosa na atatumikia adhabu hiyo kwa moyo
mmoja.


Hapo juu ndio maneno ya Suarez leo katika mtandao wake wa Twita


Suarez alijifunga kitambaa mdomoni leo katika mazoezi ya timu yake
0 comments:
Post a Comment