Red Coast, Abajalo, Friends Rangers zafuzu hatua ya Kanda
Ligi
Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imemalizika leo
kwa timu tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zimefuzu kucheza
hatua ya Kanda.
Katika
mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga Sharif Stars
mabao 2-0. Mabao hayo yamefungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya 12 na
Mwenda Athuman katika dakika ya 57.Kwa matokeo hayo Rangers imefikisha
pointi 8.
Kwenye
uwanja wa Kinesi Red Coast wameibuka na ushindi wa bao 1-0.Bao hilo
limefungwa dakika ya 32 na Rafael Mapunda. Kwa matokeo hayo Red Coast
wamefuzu hatua hiyo kwa kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligi
hiyo.
Abajalo
nao wamefuzu hatua hiyo baada ya kuichapacha Boom FC mabao 2-0. Hata
hivyo mechi hiyo ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC
kutolewa kwa kadi nyekundu.Abajalo imeweza kufuzu baada ya kujikusanyia
pointi 10.
0 comments:
Post a Comment