Klabu
yenye pesa zake Chelsea ya jijini London inaamini imeshinda mbio za
kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Garcia Falcao
Zarate, ambaye kila anapolala anaota mabao.
Mazungumzo
wakala wa nyota huyo wa Colombia, viongozi wa Atletico na kalbu ya
Chelsea yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa sasa, lakini Chelsea
wanafikiri wako karibu kumsajii.
Chelsea
sasa wanaonekana kuacha na mpango wa kutaka kumsainisha Edinson Cavan
baada ya kuwepo dalili za kumkamata Falcao ambaye anaotwa kila siku na
vijana hao wa Darajani.

Falcao
anatisha kwa mabao na kama mashine hii itawasili jijini London msimu
ujao wa ligi, mabeki wa timu za Uingereza wajiandaa kukabana na mtu
mataalamu na wasipojiangalia watamwaga unga kazini kwao.

Shangwe kubwa: Falcao akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Sevilla kwenye La Liga Jumapili

Mmiliki
wa Chelsea mwenye jeuri kubwa ya pesa, Roman Abramovich ameridhia kumpa
mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki mchezaji huyo na pia atatoa kiasi
cha Pauni milioni 46 ambazo Atletico inataka kama dau la kumuuza nyota
wake huyo.
0 comments:
Post a Comment