Na Baraka Mpenja
Wajelajela
Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya “Jiji la kijani” wanatarajia
kuanza safari yao hapo kesho kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya
mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Maafande wa jeshi la
kujenga Taifa JKT Ruvu dimba la Chamazi Mbande nje kidogo ya jiji la Dar
es salaam siku ya mei mosi mwaka huu.
Katibu mkuu wa Tanzania Prisons Sadick Jumbe ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa
kikosi chao mpaka sasa kipo salama na kimejiandaa kwa muda mrefu
kuwakabili JKT Ruvu ambao kwa sasa wana morali kubwa ya kupambana
kubakia ligi kuu msimu kutokana na kupata matokeo ya ushindi mchezo
uliopita dhidi ya vibonde wa Ligi hiyo Africa Lyon ya jijini Dar es
salaam.
“Kocha
wetu Jumanne Chale amefanya mazoezi ya nguvu kujiandaa na mchezo huo,
tuko nafasi ya tisa kati ya timu 14 tukiwa na pointi 26 sawa na
wapinzani wetu, lakini malengo yetu ni kushinda mchezo huo ili kujiweka
nafasi nzuri katika msimamo wa ligi”. Alisema Jumbe.
Katibu
huyo aliongeza kuwa kwa sasa timu ina morali kubwa kutokana na wadau wa
jijini Mbeya kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti wakiongozwa na kamanda
wa polisi mkoani humo, Diwani Athman Msuya ambaye anaongoza kamati ya
saidia Prisons ishinde.
“Tunakuja
Dar es salaam tukiwa kamili gado, lazima niwaambie mashabiki kwamba
kikosi chetu kwa sasa kipo imara na wachezaji wote wapo katika hali
nzuri, tutapambana sana na maafande wenzetu ili kupata matokeo ya
ushindi”.
Wakata
huo huo maafande wa JKT Ruvu wakiwa chini ya mwalimu Keny Mwaisabula
”mzazi” na msaidizi wake Greyson Haule wanaendelea na mazoezi kujiandaa
na matanange huo wa kukata na mundu.
Akizungumza
leo hii, Haule ambaye ni kocha msaidizi wa klabu hiyo alisema wana
uhakika wa kupata matokeo ya ushindi mbele ya Prisons kwani kikosi kipo
sawa ka mechi zote zilizosalia.
“Tuliwafunga
Lyon na kupata pointi tatu na kufikisha 26 sawa na Prisons, hakika
tunasakama kwa nguvu zote pointi nyingine tatu mbele ya wanajeshi
wenzetu, lazima tuwaadabishe siku hiyo”. Alisema Haule.
Timu
hizo mbili zote zina pointi 26 katika nafasi ya tisa na kumi, lakini
Prisons wapo juu ya Ruvu kufuatia wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa.
0 comments:
Post a Comment