Friday, April 5, 2013

SUNZU
KAZIMOTO

KIUNGO Mwinyi Kazimoto Mwitula na mshambuliaji Felix Mumba Sunzu Jr. huenda wakarejeshwa wakati wowote kuanzia sasa kwenye kikosi cha Simba SC kinachoendelea na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea nchini, imeelezwa.
Hiyo inafuatia maombi ya wachezaji walio kundini hivi sasa Simba SC kuwataka wawili hao warejeshwe kuongeza nguvu ya kikosi katika patashika ya Ligi Kuu.
“Wachezaji na baadhi ya watu wa benchi la Ufundi wameomba hawa wawili warejeshwe. Na hata wachezaji wenyewe kwa kweli wameonyesha nia ya kurejea kikosini na kuitumikia timu kwa moyo mmoja,”amesema Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga alipozungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu.
Kamwaga amesema taratibu za kuwarejesha wawili hao kundini zimeanza na ndani ya siku mbili hizi wanaweza kuanza mazoezi na wenzao.
Sunzu, raia wa Zambia mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mzalendo, Kazimoto ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Simba SC walioondolewa kwenye programu ya timu kwa sasa kutokana na utovu wa nidhamu.
Wengine ambao kocha Mfaransa Patrick Liewig hataki kuwaona ni mabeki Juma Nyosso, Amir Maftah, Paul Ngalema, Komabil Keita kutoka Mali, viungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Haruna Moshi ‘Boban’ na mshambuliaji Abdallah Juma.
Kwa sasa, Simba SC inaundwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili, wakiongezewa nguvu na wachache waliokuwa kikosi cha kwanza, mabeki Shomary Kapombe, Nassor Masoud ‘Chollo’, viungo Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
Simba inaendela na mazoezi kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam ikijiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC wiki ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa sasa, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu wanashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zao 35, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam FC 43 na Yanga walio kileleni kwa pointi zao 49, zikiwa zimesalia mechi tano tano ligi kutia nanga msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video