Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE
bendi ya nguli wa muziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa
imekamilika na anatarajia kuizindua rasmi mwezi ujao jijini Dar es
Salaam.
Ras
Inno ambaye ni mshindi wa tuzo nne za mwanamuziki bora wa reggae
Tanzania, amesema bendi yake hiyo ina wanamuziki 11 na itazinduliwa
katika hafla maalumu katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.
Amasema
nia ya kuanzisha bendi hiyo ni kuwa na ufanisi bora zaidi wa kufanya
kazi zake za muziki, kwani bendi ya kudumu na wanamuziki wa kudumu
hujenga ‘patern’ ambayo ni sawa na wachezaji waliozoeana uwanjani.
“Hiyo
hulinda ladha ya nyimbo husika kutobadilika kila show, pia uhakika wa
kufanya kazi njema nje ya nchi. Lakini pia kuwa na bendi huhakikisha
upatikanaji wa tija ya kudumu, tofauti na ukiwa ‘solo’ tu bila jina la
bendi kazi huja kwa misimu kutokana na mazoea ya hapa kwetu Bongo,”
amesema.
Amesema
bandi hiyo ni mojawapo ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa taasisi
yake mahsusi ya kuupromoti muziki wa reggae, kwa ushirikiano na wadau
wengine miongoni wa mitindo mingine kwa kuzingatia weledi.
“Taasisi
inaitwa Reggae Production House ambayo itahakikisha uzalishwaji wa
vipaji vipya vya vijana wanaotaka kuingia kwenye reggae, kwa kufuata
njia sahihi itakayowajenga kuwa wanamuziki bora wa reggae nchini
watakaoweza kufanya kazi kimataifa.
“Dhima
nzima ni kuufufua muziki wa reggae hapa nchini si kwa kuwa umekufa, la
hasha, ila kuna mazingira yanayoufanya muziki huu uonekane kama haupo,
lakini mahitaji yapo na mashabiki wana hamu kubwa nao.”
Aidha
ameongeza kusema kwamba, ukimya wake wa muda mrefu una sababu kadhaa
zikiwemo za kibinafsi kimaisha, lakini muda aliokuwa nje ya ulingo,
ameyasoma vyema mazingira yanayoukabili mtindo wa reggae hivyo naamini
ana dozi ya kuutibu.
0 comments:
Post a Comment