![]() |
KENY MWAISABULA "MZAZI" |
Na Baraka Mpenja
Wakati
maafande wa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani wakihaha kujinusru kubakia
ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu 2012/2013, kocha wake mpya Keny
Mwaisabula “Mzazi” amesema malengo yake makubwa ni msimu ujao kwani kwa
sasa hana uwezo wa kubadili kikosi chake.
Akizungumza na MICHEZO BOMBA!
leo hii, Mwaisabula ambaye timu yake ilipoteza mchezo wake muhimu jana
kwa kufungwa na vinara Yanga mabao 3-0 alisema amekubali majukumu ya
kuinoa klabu hiyo na taratibu zote za mkataba wake zimekamilika.
“Kwa
sasa ninahusika kutoa ushauri kwa timu yangu kwani ndio kwanza nimeanza
kazi, hakika muda huu hautoshi kwangu hivyo najiandaa na msimu ujao wa
ligi”. Alisema Mwaisabula.
Kocha
huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati inayoratibu sherehe za mei mosi
mwaka huu zitakazofanyika kitaifa jijini Mbeya, aliongeza kuwa licha ya
timu yake kuwa na pointi 23 katika nafasi ya 11 ya msimamo wa ligi kuu
bara, mategemeo yake ni kufanya vizuri mechi zilizosalia ili
kujihakikishia nafasi ya kubakia ligi kuu.
“Tunajiandaa
na mchezo wa keshokutwa dhidi ya Africa Lyon, tumepoteza jana dhidi ya
vinara Yanga, sasa hesabu zetu ni kupata pointi tatu ili kufikisha 26 na
kuendelea kujiweka salama, wachezaji wapo salama na wana morali ya
kuikoa timu yao”. Alisema Mwaisabula aliyewahi kuifundisha Yanga.
Aidha
Kocha huyo aliyewahi kuzifundisha klabu za Africas Lyon, Villa Squad,
na nyinginezo aliwataka mashabiki wa soka mkoani Pwani kuondoa hofu
kwani watajitahidi kufanya vizuri zaidi ili kuwafurahisha msimu ujao.
Mwaisabula amerithi mikoba ya kocha aliyebwaga manyanga kuwanoa maafande hao wa JKT Ruvu, Mwalimu Charles Kilinda.
0 comments:
Post a Comment