![]() |
Musa Hassan Mgosi Kulia |
Na Baraka Mpenja
Nguli wa kusakata kabumbu na aliyewahi
kutamba na klabu ya Simba, DC Mote Mapembe ya Kongo na sasa yupo na JKT
Ruvu Musa Hassan Mgosi “Mgunya” amesema kesho ni kesho lazima awapoteze
Lyon kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndani ya dimba la
Chamazi mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam dhidi ya klabu ya
Africa Lyon.
Mgosi ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa
anajisikia vibaya sana timu yake kufungwa na Yanga 3-0, na sasa hesabu
zake ni kufuta machungu hayo mbele ya wapinzani wao wakubwa katika
mchezo wa kesho.
“Endapo Lyon watatufunga watakaa juu
yetu, na sisi tukipata matokeo ya ushindi tutajiweka mahali pazuri,
wachezaji wote tunajua wajibu wetu na kesho ni shughuli moja ya kutafuta
ushindi tu”. Alisema Mgosi.
Nyota huyo mwenye uchu wa kufunga
magoli aliongeza kuwa yeye ni mchezaji mwenye mbinu nyingi za kufumania
nyavu na kesho itatumia mbinu zake za Kongo na simba miaka ya nyuma
kuwazamisha Lyon.
“Mara nyingi natumia muda wangu
kuwaambia wachezaji wenzangu kuwa soka lina matokeo matatu, kufunga,
kufungwa na kutoa sare ama suluhu, tukifungwa tunayaacha uwanjani na
kwenda kujifua upya, nafikiri wamenielewa na kesho tutacheza kwa
ushirikia’.
0 comments:
Post a Comment