Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Wakati
miamba ya soka la Hispani, Real Madrid wakikabiliwa na kibarua kizito
hapo kesho kuhitaji ushindi wa mabao 3-0 mbele ya nyuki wa kaskazini
mashariki mwa Ujerumani, Borussia Dortmund, katika mchezo wa fainali ya
pili ya Ligi ya mabingwa barani ulaya, mshambuliaji wa zamani wa Man
City, sasa akikipiga AC Milani na timu ya taifa ya Italia “The Azzuri”,
Mtukutu Supa Mario Balotell ametoa kali baada ya kumtumia mpenzi wake
Mbelgiji Fanny Neguesha kuwakebehi Real Madrid kuelekea kipute cha
kesho.
Balotell
amesema ana imani kubwa Dortmund watafuzu hatua ya fainali na kama Real
Madrid watawatoa katika mchezo wa kesho na kucheza fainali Wembley
mwaka huu basi atawapa idhini ya kulala na mpenzi wake kwa usiku mzima.
Mgazeti
ya Hispania ya AS NA Marca yamemkariri nyota huyo wa AC Milan akisema
“Kama Real Madrid watafuzu fainali ya UEFA mwaka huu baada ya kufungwa
4-1, nitawaachia mpenzi wangu alale nao”.
Akitabasamu:
Mario Balotelli akishangilia baada ya kuzamisha gozi kambani kwa njia
ya mkwaju wa penato dhidi ya Catania usiku wa jana.
Mpenzi
wa Balottell Fanny Neguesha ambaye amechora Tattoo ikieleza hisiza
zake za kimapenzi kwa Balotell, endapo Madrid watafuzu mtoto mzuri yupo
kwa ajili yao leo
Balotelli na Neguesha mahusiano yao yamejengeka zaidi baada ya nyota huyo kuihama City na kuhamia AC Milani.
Dortmund waliwatandika kipigo cha Mbwa mwizi Real Madrid huku Robert Lewandowski akipiga goli zote nne.Manchester United na Bayern Munich zote zinaitaka saini ya Lewandowski.Cristiano Ronaldo ambaye alufunga bao moja la kufutia machozi wikiendi iliyopita alikosa mchezo wa timu yake dhidi ya Atletico Madrid kufuatia kuwa majeruhi, lakini leo amefanya mazoezi na kocha Mourinho amefurahishwa na kurejea kwa nyota wake.

Robert Lewandowski atafanya nini Santiago Berbeu usiku wa kesho
Wachezaji wa Real Madrid |
0 comments:
Post a Comment