
Mshambuliaji
mwenye shabaha kubwa ya kufunga mabao anayekipiga darajani Chelsea raia
wa Senegal Demba Ba, amemtaka kocha wake, Rafa Benitez awapange yeye na
Fernando Torres katika safu ya ushambuliaji kesho katika mechi ya Ligi
Kuu ya England dhidi ya Liverpool.
Benitez
ambaye amekuwa akiwazungusha wachezaji hao katika mfumo wa 4-2-3-1
tangu Ba ajiunge nao kutoka Newcastle Januari mwaka huu, lakini
wakicheza pamoja walifanya vizuri kipindi cha pili wiki iliyopita katika
Nusu Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City.
Benitez
anakabiliwa na kigugumizi cha kuamua kuhusu kikosi chake, akiwa hana
imani na kumuanzisha Torres dhidi ya timu yake ya zamani na kwa kiwango
cha Ba inamfanya adharau kabisa, lakini Msenegali huyo amesema wanaweza
kucheza pamoja.
Pacha uwanjani? Demba Ba (kushoto) anataka kucheza pacha na Fernando Torres katika safu ya ushambuliaji Chelsea
0 comments:
Post a Comment