Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hatimaye
timu zote za Ujerumani, Bayern Munich na Borussia Dortmund zimetoka
kidedea katika michezo yao ya kwanza ya nusu fainali ya ligi ya mbaingwa
barani ulaya baada ya kuzitandika timu za Hispania Barcelona na Real De
Madrid vipigo vya mbwa mwizi.
Leo
hii kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa timu bora ilipta
ushindi hapo jana wala hana tatizo lolote kwa kiwango cha wajerumani
hao.
Mourinho alisema anatarajia miijuzi mechi ya marudiano wiki ijayo huko Santiago Berbeu.
Robert
Lewandowski, mshambuliaji hatari toka Poland ambae ni wazi anaihama
Borussia Dortmund mwishoni Msimu huu kuelekea ama Bayern Munich au
Manchester United, jana usiku alitandika Bao 4 na kuiteketeza Real
Madrid Bao 4-1 Uwanjani Signal Iduna Park Jijini Dortmund katika Mechi
ya kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hiki
ni kilio cha pili kikubwa kwa Spain Nchini Germany katika Mashindano
haya baada ya Jana Barcelona kuwashwa Bao 4-0 na Bayern Munich Uwanjani
Allianz Arena huko Jijini Munich katika Nusu Fainali nyingine.

Muuaji wa Madrid Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuwatungua Madrid bila aibu
Maskini : kocha wa Real Madrid Jose Mourinho
Cristiano Ronaldo akitafakari jambo baada ya kupigwa kipigo chA mbwa mwizi



Lewandowski akitia kimiana moja ya magoli yake hapo jana

Utampenda Lewandowski hili ni moja kati ya bao alilofunga kwa ufundi mkubwa sana

Hapa anashangilia kwa hisia kubwa sana

Cristiano Ronaldo akiisawazishia Real Madrid kabla ya mapumziko

Ronaldo akishangia bao pekee alilofunga hapo jana


Wachezaji wa Borussia wakipongeza kwa kutoa kisago kwa Real Madrid


Wauaji wa Madrid wakipongezana

Lewandowski akipiga mkwaju wa penati na kuandika bao la nne na la mwisho kwake
0 comments:
Post a Comment