![]() |
JULIO KUSHOTO AKIWA NA MSEMAJI WA SIMBA EZEKIEL KAMWAGA |
Na Baraka Mpenja
Wekundu
wa Msimbazi Simba leo wana kibarua kizito uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam pale watakapokuwa wanaoneshana kazi na vijana wa Charles
Boniface Mkwasa “Master” klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi
kuu soka Tanzania bara.
Mchezo
huo unatarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana na ukweli kwamba Simba
kwa sasa wanahitaji kulinda heshima yao baada ya kupoteza taji lao
msimu huu na kuwapa mahasimu wao wa jadi, Dar Young Africans, wakati nao
Shooting wanahitaji kupata pointi tatu muhimu ili kujiweka nafasi nzuri
zaidi katika msimamo.
Akizungumza
na mtandao huu, Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kiwhelo “Julio” alisema
kikosi cha Simba kipo salalama na leo kama ilivyo kawaida kwao vijana
wengi wataanza kikosi cha kwanza kupepetana na wanajeshi hao.
“Simba
iko safi na sasa tunajenga wachezaji, kocha anatarajia kuwapanga vijana
wadogo kama kawaida na tunaamini watacheza soka maridhaWa kama
walivyofanya mechi za nyuma”. Alisema Julio.
Julio
aliwataja baadhi ya nyota wao makinda wanaotaraji kucheza katika mechi
ya leo ya kukata na shoka maeneo ya Chang`ombe uwanja wa taifa.
“Unajua
kwa sasa huwezi kuitaja simba bila kuwataja akina Kapombe, Seseme,
Singano, Chanongo na wengine wengi, lakini pia tutatumia baadhi ya
mafaza kuiwakilisha Simba ambayo kwa sasa tumepoteza ubingwa ila
tunahitaji heshima”.
Julio aliwataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kwani kikosi kipo na morali kubwa.
Kwa uande wa Shooting walisema wamekamilisha taratibu zote za kumfunga mnyama.
Akizungumza
kwa kujiamini Afisa habari wa klabu huyu Masau Bwire alisema licha ya
Simba kutangaza kulinda heshima katika mechi zilizosalia, lakini wao
wanajua kuwa lazima wawafunge katika mechi ya leo.
“Sisi
tuko sawa usipime, kocha Mkwasa na Suleiman Msungwe wamewaandaa vijana
kwa kushindana, leo lazima mnyama afanyiwe kitu mbaya taifa, Shooting ni
timu nzuri na wao wanajua sana shughuli yetu, tunataka watanzania
walijue hilo”. Alisema Masau.
0 comments:
Post a Comment