Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Mashindano
ya vijana chini ya miaka 14 na 20 yanayoratibiwa na chama cha soka la
vijana wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam yamesogezwa mbele ambapo
sasa yataanza kutimua vumbi mei 4 badala ya mei mosi mwaka huu katika
dimba la kumbukumbu ya Hayati Karume.
Mwenyekiti wa chama cha soka la vijana Ilala (IDYOSA) Faza Edwirn Mloka ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa
katika kikao cha kamati yan mashindano kilichofanyika hivi karibuni
timu shiriki ziliomba kusogezwa mbele ili kuwaandaa vizuri vijana wao,
na wao wamekubaliana nao na kutoa nafasi hiyo kwao.
“Klabu
zimeomba kujiandaa vizuri na sisi tumesogeza siku, hapo kesho mei mosi
tunakutana ofisi za TFF karume saa tatu asubuhi kupanga ratiba ambapo
makocha na makatibu wa timu watahusika”. Alisema Mloka.
Mloka alisema mwaka huu wanatarajia kuendesha mashindano yenye mvuto zaidi na kufuata kanuni zilizowekwa na chama hicho;
“Hatutaki
vijeba katika michuano hii, tumefanya usaili makini sana wa wachezaji,
kila atayecheza ana umri sitahiki na hivi ndivyo tunavyotaka, hakuna
shaka kila kitu kitaenda shwari”. Alisema Faza Mloka akiwa na uhakika.
Pia
mwenyekiti huyo aliwataka wadau na wapenzi wa kandanda kutupia macho yao
katika mashindano haya kwani ndio chimbuko la baadhi ya wachezaji
wanaofanya vizuri sana ligi kuu soka Tanzania bara.
“Huwezi
kumtaja bwana mdogo Salum Abubakar “Sure boy” au Frank Domayo wa Yanga
bila kuhusisha michuano ya vijana Ilala, hapa ndio chimbuko la nyota
hawa na wengine wengi, ni muhimu kujitokeza kuwasaidia vijana wetu”.
Alisisitiza Mloka.
Baada
ya michuano hii chama cha soka manispaa ya Ilala kimealikwa mwezi juni
mkoani Tabora kushiriki michuano ya vijana ya mkoa huo kama sehemu ya
kubadilishana uzoefu wa uongozi wa soka la vijana pamoja na kudumisha
umoja na mshikamano.
Soka
la vijana kwa sasa ndio msingi wa soka duniani kote na kila taifa sasa
linawekeza huko, huku Tanzania pia tukifuata nyayo zao tukiongozwa na
Rais wa TFF anayemaliza muda wake Injinia Leodigar Chilla Tenga ambaye
hivi karibuni ametoa mipira 1200 iliyogharimu dola elfu tatu ili igawiwe
shule za misingi na vituo vya soka mikoa yote ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment