THOMAS MASHALI
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, anatarajia kuondoka nchini leo kwenda Afrika Kusini ‘Bondeni’ kwa ajili ya kuweka kambi ili kujiandaa na pambano la kuwania ubingwa wa IBF Afrika dhidi ya Francis Cheka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mashali alisema anatarajia kuondoka nchini leo kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo, ambalo linatarajiwa kufanyika Mei Mosi kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mashali alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo na kudai atahakikisha anachukua ubingwa huo kutokana na maandalizi ambayo anaendelea kuyafanya hivi sasa.
“Kiukweli nipo vizuri zaidi ya sana na kesho natarajia kuondoka kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo, ambalo naamini nitamvua Cheka mkanda huo,” alisema Mashali.
Bondia huyo ambaye ana historia ya kutopigwa katika mapambano yake, aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuangalia pambano hilo ambalo litakuwa na ushindani mkubwa.
Ubingwa wa IBF Afrika kwa sasa unashikiliwa na Cheka ambaye pia amesema amejiandaa vema kuutetea.
FRANSIS CHEKA

0 comments:
Post a Comment