Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Kwa
mara ya kwanza nyota wa Manchester united na timu ya taifa ya Uholanzi,
Robin Van ersie “RVP” atashusha daluga zake katika dimba la Emirates
tangu aihame klabu hiyo.
RVP
ambaye alifunga mabao matatu “Hat Trick” dhidi ya Aston Villa na kuwapa
United ubingwa wa 20 wa ligi kuu soka nchini Uingereza atarejea nyumbani
huku akikumbukwa na mashabiki wengi wa Arsenal jijini London.
Nyota
huyo alikuwa kipenzi cha wana Arsenal lakini alikataa kusaini mkataba
na klabu hiyo kwa madai ya kuhitaji timu ambayo atatwaa kombe ili
kujijengee heshima katika maisha yake ya soka.
Na
mpaka sasa amefanikisha ndoto zake na sasa anaenda kupambana na watu
wake wa karibu majira ya saa 12 jioni ambao alicheza nao kwa miaka 8 na
baadaye kuihama kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 24.

RVP alisema “Sitarajii hali yoyote tofauti na presha ya mashabiki wa Arsenal, lakini siumizi kichwa hata kidogo kwani katika soka ni kawaida”.
Nyota huyo mwenye uchu wa kupachika mabao mpaka sasa anaongoza kwa kutia gozi kambani akiwa ameshafunga mabao 24 na anaweza kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu akiwa na United.
Msimu wa mwaka jana alifanya hivyo akiwa na Arsenal ambayo aliihama kwa pauni milioni 24 kwa lengo la kutafuta mataji na mwaka huu amepata taji la kwanza nchini humo.
Akizungumza na gazeti la jumapili la The Sun, Van Persie aliongeza kuwa siku zote anawaheshimu mashabiki wa Arsenal na anajua wanavyoipenda timu yao, hivyo hana tatizo nao.
Msimamo wa timu tano za juu baada ya michezo ya jana


Van
Persie akiwa Arsenal enzi hizo na jumatatu ya wiki alifunga “Hat Trick”
katika mchezo uliowapa Man U ubingwa wa 20 wakiwa na kocha Mscotish
Alexandar Chapman Ferguson maarufu kama Kibabu Fergie.

RVP
aliendelea kusema kuwa anaangalia mbele tu na leo hii anatarajia
kuonana na marafiki zake kwa mara ya kwanza tangu aihame klabu hiyo
pamoja na viongozi wake.
Kibabu
Sir Alex Ferguson leo hii anaweza kuwapumzisha baadhi ya nyota wale
akiwa ameshatwaa ndoo na Van Persie alisema hana uhakika wa kucheza
ingawa anapenda kucheza kila mechi ila maamuzi yapo chini ya kocha wake.

Mashabiki
wa Arsenal wakiwaonesha bango lenye maandishi yenyen maana ya
“TUNAMPENDA VAN PERSIE” katika moja ya mechi alizocheza nyota huyo mwaka
2009
Wakati
huo huo kocha wa Arsenal mfaransa, Wenger anaamini kuwa United
ingetwaa ubingwa wake wa 20 mwaka huu bila kuwepo kwa RVP.
Nahodha
huyo wa zamani wa washika bunduki wa London, anatajwa kuwa na mchango
mkubwa sana katika ubingwa wa United ambao wamewapoke watani wao wa jadi
Man city.

Wenger alisisitiza kuwa mabao ya RVP sio sababu pekee ya united kutwaa mzigo wa ligi kuu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment