![]() |
Msanii wa Nguli wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule “Profesa J” atakuwepo siku ya Maji Maji day |
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Tamasha
la siku ya Maji Maji “Maji maji Day” lililotarajiwa kufanyika Aprili 27
mwaka huu mjini Songea kwa lengo la kuwachangia wanandinga wa klabu ya
majimaji “Wanalizombe” limesogezwa mbele mpaka mwezi juni mwaka huu ili
kupisha uchaguzi wa viongozi klabuni hapo.
Akizungumza kwa njia ya simu na MICHEZO BOMBA! kutoka mjini Songea, meneja wa klabu hiyo Godfrey Ambrose Mvula maarufu
kama Makete alisema kwa mujibu wa katiba yao uongozi unatakiwa kukaa
madarakani kwa miaka minne lakini uongozi wa sasa upo madarakani kwa
miaka mitano kinyume na katiba halali ya klabu.
“Hatuna
jinsi, tumeshauriana na wadau wetu na kuamua kufanya uchaguzi ili
kupata viongozi wapya watakaoshirikiana na wadau kuendesha tamasha hilo
mwezi wa sita, hivyo tunafanya mipango ya uchaguzi kati ya mei 15 hadi
20 mwaka huu”. Alisema Makete.
Makete
alizitaja nafasi zitakazowania katika uchaguzi huo kuwa saba kwa maana
ya mwenyekiti na makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe watano wa bodi ya
klabu hiyo.
Baada
ya kufanya uchaguzi meneja huyo alisema wataendelea na mchakato wa
kuzungumza na wadau mbalimbali wa klabu hiyo wakiwemo wachezaji wote
waliowahi kukipiga kwa wana Lizombe hao wa Songea kufanikisha tamasha
hilo.
Makete
amewataja baadhi ya nyota wa zamani wanaotarajiwa kuwepo katika tamasha
hilo la kuchangia klabu hiyo kuwa ni Idd Pazi Faza, Willy Martin, Amri
Said “Jap Stam”, Ibrahim Mbuzi, Abdallah Waswa kutoka Kigoma, Steven
Mapunda “Garincha” na wengine wengi.
Pia
aliongeza kuwa watamwalika winga machachari wa zamani wa klabu ya Simba
na kocha wa wana “Nkulukumbi” Kagera sugar, Abdallah King Kibaden Mputa
pamoja na mzee wa kiminyio Madaraka Seleman.
Pia
Makete aliongeza kuwa tamasha hilo linatarajia kupambwa na burudani ya
muziki utakaoongozwa na wasanii wenye asili ya Ruvuma akiwemo nguli wa
muziki wa kizazi kipya Joseph Haule “Profesa Jay”.
0 comments:
Post a Comment