Wachezaji
wa klabu ya Yanga ambao ndio mabingwa wa liku kuu soka Tanzania bara
msimu wa 2012/2013 wakiweka miili sawa, wa kwanza kulia ni kiungo
tegemeo wa klabu hiyo Mnyarwanda Haruna Hakizima Fadhil Niyonzima
maarufu kama Fabrigas, naye atakuwepo hapo kesho kupambana na wagosi wa
kaya
Kikosi
cha Wagosi wa kaya, Wagosi wa Ndima kutoka jiji la Tanga, hawa ndio
walichangia kuwapa ubingwa Yanga wiki hii baada ya kuwabana Azam, sasa
wanashuka ugani kesho dhidi ya mabingwa hao
Na Baraka Mpenja
Wakiwa
tayari mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013,
wanajangwani Dar Young Africans wamesema mchezo wao wa mei mosi dhidi ya
wagosi wa ndima wagosi wa kaya Caostal Union kutoka jijini Tanga “waja
leo waondoka leo” ndani ya dimba la kisasa la taifa jijini Dar es salaam
utakuwa maalumu kwa mashabiki wa klabu huyo kufurahia pamoja ubingwa
wao huku timu yao ikiwa inaendelea kufanya vizuri.
Afisa habari wa mabingwa hao waliotwa taji mara 24 liku kuu, Baraka Kizuguto ameiambia MICHEZO BOMBA!
kuwa baada ya kuwapoka ubinwgwa watani zao wa jadi, sasa wanataka
kuwafurahisha mashabiki wao katika michezo yao miwili iliyosalia.
Yanga
wamebakiza mechi mbili baina ya Wagosi wa Kaya ambao watakwaruzana nao
kesho taifa na mchezo wa mwisho utawakutanisha na watani zao wa jadi
wekundu wa msimbazi Simba wenye kumbukumbu ya kuwachapa kipigo cha mbwa
mwizi cha mabo 5-0 msimu wa mwaka jana.
“Licha
ya kuwa mabingwa Yanga hatubweteki hata kidogo, tunaanza kugawa dozi
kwa wagosi wa kaya na baada ya hapo tunaanza kuwawinda Simba ambao
kuwafunga itaongeza raha ya ubingwa wetu”. Alisema Kizuguto.
Kuhusu
hali ya wachezaji, Kizuguto alisema wote wapo salama na wana morali
kubwa sana kuwavaa wapinzani wao waliochangia kuwapa ubingwa baada ya
kuwabana waliokuwa wapinzani wao wakubwa Azam fc “Lambalamba” kwa
kutoka nao sare ya bao 1-1 dimba la chama cha Mapinduzi (CCM) jijini
Tanga.
“Tumefanya
mazoezi vizuri, wachezaji kwanza wana furaha ya kutwaa ubingwa, lakini
wanaahidi kuwa ili kunogesha utamu wa ubingwa wao lazima washinde kesho
na mechi ya Simba”. Alisema Kizuguto kwa kujiamini.
Wakati
Yanga wakitamba kuibuka kidedea hapo kesho, kwa upande wa Coastal union
wamesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Hemed Morroco ameimabia MICHEZO BOMBA!
kuwa licha ya waamuzi kuvurunda baadhi ya michezo wao wamejipanga kwa
uzuri sana kukabiliana na Yanga hapo kesho uwanja wa taifa.
“Siku
tumecheza na Azam nyumbani waamuzi walichemsha sana na kusababisiha
tushindwe kupata ushindi, hakika tulistahili kuwafunga, sasa tuna kazi
nyingine na Yanga sijui itakuwaje, lakini tumejipanga kwa lolote lile”.
Alisema Morroco kwa kujiamini.
Coastal
union wamejikusanyia pointi 36 katika nafasi ya tano, juu yao wapo
Simba wenye pointi 39 katika nafasi ya nne huku Kagera Sugar wakiwa
nafasi ya tatu na pointi 40 na Azam wapo nafasi ya pili na mzigo wa
pointi 48.
Kesho
mashine za Yanga kama Haruna Niyonzima “Fabrigas”, Khamis Kiiza, Saimon
Msuva, Athman Idd “Chuji”, Frank Domayo, Kelvin Yondan, Canavaro na
wengine wengi wataongoza kikosi chao kupepetana na Wagosi wa ndima
kutoka Tanga.
0 comments:
Post a Comment