Na Baraka Mpenja
Waburaza
mkia wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Africa Lyon ya jijini Dar
es salaam sasa wameanza kujiandaa kucheza ligi daraja la kwanza baada
ya kupumua kwa mashine dakika hizi za lala salama.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Mkenya Charles Otieno ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa
timu yao sasa ina aslillimi tano kati ya mia moja kuabkia ligi kuu huku
wakiongoza kwa kufungwa mabao mengi zaidi ya timu zote.
Otieno
alisema hali yao ni ngumu sana hivyo wanajipanga kwa lolote kwani
katika mechi mbili zilizosalia wanaweza kufikisha pointi 25 pamoja na
wapinzani wao polisi morogoro,na Toto Africans, lakini Mgambo akipata
moja tu hawa ujanja.
“Ukiangalia
jinsi ligi inavyokwenda endapo Mgambo atapata pointi moja katika
michezo yake iliyosalia, basi sisi, Toto na Polisi ndio hivyo tutaenda
kujipanga ligi daraja la kwanza”. Alisema Otieno.
Kocha
huyo aliongeza kuwa timu haina matatizo makubwa sana lakini kubwa zaidi
ni sehemu ya ushambuliaji ambayo inapata nafasi nyingi na kushindwa
kuzitumia.
Otieno
alisisitiza kuwa watu wengi wanaona itakuwa vibaya sana kurudi ligi
daraja la kwanza, lakini kiukweli hawana jinsi na lazima wajiandae
kulingana na msimamo ulivyo.
“Mimi
nitabaki na timu mpaka mwisho, tukishuka daraja tutajipanga ndani ya
mwaka mmoja na kurudi ligi kuu tena, timu ina hela za kuwalipa wachezaji
mishahara, posho, usafiri na mtu akisema tuna matatizo ya pesa sio
sahihi”. Alisema Otieno.
Akiongelea
saula waamuzi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Otieno alisema waamuzi
wengi wanachezesha ovyo na kushindwa kutafsiri kwa ufasaha sheria 17 za
kandanda.
Lyon
mpaka sasa ipo mkiani ikijikusanyia pointi 19 na dalili zote
zimeshawadia, wanaweza kushuka daraja na kupisha timu za Mbeya City,
Rhino Rangers na Ashanti United zilizopanda daraja msimu huu.
0 comments:
Post a Comment