![]() |
Musa Hassan Mgunya "Mgosi" kulia, ataongoza safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu |
Na Baraka Mpenja
Ligi kuu Tanzania bara inatarajiwa
kuendelea leo kwa mechi moja kuchezwa katika dimba la Chamazi baina ya maafande
wa JKT Ruvu kutoka Pwani dhidi ya Africa
Lyon ya jijini Dar es salaam.
Kuelekea katika mchezo huo unaowakutanisha
wapambanaji wa kukwepa rungu la kushuka daraja msimu huu timu zote zimeiambia MICHEZO BOMBA! kuwa zimejipanga kuibuka
kidedea katika mchezo huo wa kukata na shoka.
Katibu mkuu wa Africa Lyon Ernest
Brown alisema hawana cha kupoteza zaidi ya kutafuta ushindi mbelebya wareruhiwa
JKT Ruvu ambao mchezo uliopita waliambulia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa
vinara Yanga uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
“Hali yetu ni mbaya sana msimu huu,
tuko hatarini kushuka daraja, mchezo wa leo tumejiandaa kushinda ili kupata
pointi tatu muhimu mbele ya wapinzani wetu”. Alisema Brown.
Brown alisema msimu huu ligi imekuwa
na changamoto kubwa sana kutokana na timu zote kushindana kwa nguvu kuhitaji
matokeo mazuri.
Katibu huyo aliongeza kuwa mashabiki
wa klabu hiyo wasife moyo kwa sababu hilo ndio soka, cha msingi na muhimu
wajitokeze kuwapa sapoti leo Chamazi ili angalau wapate pointi tatu muhimu.
Kwa upande wa JKT Ruvu, kocha wake
Mpya Keny Mwaisabula ambaye hayupo jijini Dar kwa majukumu ya kikazi alisema
timu yake iko shwari kuwavaa Lyon ambao wanahitaji kupata ushindi wa ili
kujinusuru na mkasi wa kushuka daraja kama ilivyo kwao.
Mwaisabula alisema amepewa timu siku
za kiama lakini atahakikisha anashinda mechi zilizosalia ili kubakia ligi kuu
msimu ujao.
“Najua wengi hawaamini kama tunaweza
kusalia ligi kuu, sisi ni wapiganaji sana na tunaweza kufanya maajabu,
tumejipanga vizuri.
Na hapo kesho Wekundu wa Msimbazi
watakuwa kibaruani dhidi ya maafande wa Ruvu shooting katika dimba la taifa
jijini Dar es salaam.
Simba wameshapoteza Ubingwa ambao kwa
aslimia 99 watani zao wa jadi Dar Young Africans wapo mbioni kuunyakua kutokana
na kuhitaji pointi moja tu katika michezo miwili iliyobakia.
0 comments:
Post a Comment