Miss Tabata 2012 Noela Michael |
Na Mwandishi Wetu
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu
wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni
ya aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka
huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.
“Warembo
wazuri wamejitokeza zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya
nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema
mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.
Warembo
hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma
Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22),
Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth
Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19),
Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema
Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine
ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida
Mandali (21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga
(19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray
Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
“Bado
milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo
anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,”
mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
0 comments:
Post a Comment