Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora
imeendelea leo kwa michezo mitatu, ambapo kwenye Uwanja wa Kinesi, Abajalo imeifunga
Friends Rangers bao 1-0. Bao hilo limefungwa na Waziri Omary katika dakika ya
35. Abajalo sasa wamefikisha pointi 7 wakishika nafasi ya pili.
Kwenye Uwanja wa Makurumla, Boom FC imetoka sare ya bao 1-1
na Read Coast. Bao la Red Coast limefungwa na Idrisa Pandu katika dakika ya 28
wakati lile la Boom limefungwa na Janka Ally katika dakika ya 41.Red Coast
wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 8.
Kwenye Uwanja wa Airwing, Sharif Stars imeibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Day Braek. Bao hilo limefungwa na Dovan Kanyinda katika dakika
ya 89 na hivyo kufikisha pointi 6 katika michezo minne iliyocheza.
Kila timu hadi sasa imecheza michezo minne na ligi hiyo
itafikia tamati Aprili 27 ili kupata timu tatu za juu zitakazocheza hatua ya
Kanda.
Imetolewa na Mohamed Mharizo
Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaan (DRFA)
0 comments:
Post a Comment