USHINDI wa Manchester United dhidi ya Aston Villa 3-0 jana Uwanja wa Old Trafford, umewapa taji la 20 la Ligi Kuu ya England, wakiwapiku wapinzani wao, Manchester City waliokuwa wanashikilia taji hilo.
Shukrani
kwake mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie
aliyefunga mabao yote matatu kipindi cha kwanza na kukiwezesha kikosi
cha Sir Alex Ferguson kuibuka mabingwa kwa mara nyingine tena.
Ferguson aliongoza sherehe za ubingwa katika chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Old Trafford. Cheki picha za pati hilo.


Kibabu Ferguson akipiga mvinyo baaada ya kutwaa ubingwa wa 20 wa ligi kuu soaka nchini UingerezA jana usiku

Kikosi cha kazi cha mashetanai wekunu wakishangilia ubingwa wao wa 20 katika chumba cha kuvalia ngu0

Rio Ferdinand akirusha fataki kama ishara ya kushangilia ubingwa wakati Chicharito na Carrick wakiangalia.

Nyota
wa United, Mholanzi Robin Van Persie akionesha jezi yake namba 20
katika chumba cha kuvalia nguo baada ya kuongoza timu yake kutwaa
ubingwa wa 20 wa ligi kuu England.


Patrice Evra akitoa ulimi wake nje kama ishara ya kushangilia ubingwa huku akiwa amevaa sikafu ya ubingwa

Ubingwa: Ubao wa matangazo ya mabao dimbani OT ukiwa umebadilisha na kuandikwa united mabingwa


Sir Alex Ferguson akisalimiana na kocha msaidizi wake Mike Phelan baada ya filimbi ya mwisho

Nahodha wa united Patrice Evra akishangilia ubingwa

Rio Ferdinand aliweka picha hii kwenye akaunti yake ya Twita

Rafael and Rio Ferdinand wakipiga picha ya pamoja

Robin van Persie akifungwa bao la kwanza dakika ya 2 ya mchezo kipidni cha kwanza

Bao la pili la RVP

Bao la tatu la RVP
0 comments:
Post a Comment