![]() |
KOCHA JULIO KUSHOTO, KULIA NI MSEMAJI WA KLABU HIYO EZEKIEL KAMWAGA |
Na Baraka Mpenja
Kocha
msaidizi wa wekundu wa msimbazi Simba “Taifa Kubwa”, Mzalendo Jamhuri
Kiwhelo “Julio” amesema licha ya kupoteza ubingwa wao msimu huu na
nafasi ya pili bado wanajiandaa kwa nguvu zote kulinda heshima katika
michezo iliyosalia hasa mtanange wa funga dimba dhidi ya watani wao wa
jadi Dar Young Africans.
Julio ameiambia MICHEZO BOMBA!
kuwa kwa sasa wanaendelea kukifua kikosi chao kilichojaa makinda wengi
kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting aprili 25
uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
“Kwanza
lazima tumshukuru mungu kwa kile tulichokipata, watani wetu kwa
asilimia 99 wameshakuwa mabingwa, hata nafasi ya pili ni ngumu sana
kuipata kwetu sisi, lakini tutakapokutana na Yanga kazi ni kuwafunga ili
kupunguza machungu”. Alisema Julio.
Kocha
huyo mwenye maneno mengi aliongeza kuwa kitendo cha kocha mkuu wa klabu
hiyo Mfaransa Patrick Liewig kuwapanga zaidi vijana kuliko mafaza wa
klabu hiyo hakimaanishi hawajui kucheza, lakini mwalimu imeona hakuna
tofauti yoyote kati ya vijana na wakongwe hao.
Julio
alisisitiza kuwa kwa sasa wanaendelea na zoezi la kuwajenga mayoso wao
wanaoonekana kukua siku hadi siku na kama wataendelea kuwa na nidhamu
wanayoionesha sasa, hakika msimu ujao Simba itakuwa kali zaidi ya
kawaida.
“Tumeteleza
na kupoteza ubingwa, wana Simba hatuna haja ya kuvurugana, tuwe na
subira, simba hii ya vijana hakika itafanya vizuri sana na kuwashangaza
wengi”. Alisema Julio.
Akizungumzia
hali ya wachezaji wa Simba, Julio alisema wote wapo salama na
wanajiandaa na mchezo ujao kupepetana na wanajeshi wa Charles Boniface
Mkwasa.
Simba
ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 36 na mbele yao wapo Kagera Sugar
wenye pointi 40 na nafasi ya pili wapo Azam fc wenye pointi 47 wakati
Vinara Yanga wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 56 huku wakisubiri
kupata pointi moja tu kujitangazia ubingwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment