![]() |
Maafande wa JKT Ruvu wakimkumbuka Mungu wao |
Na Baraka Mpenja
Baada
ya kufumuliwa mabao 3-0 na vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara Dar
Young Africas, leo hii maafande wa JKT Ruvu wamepunguza machungu baada
ya kuwatungua vibonde wa ligi hiyo Africa Lyon bao 1-0 mchezo uliopigwa
dimba la Chamazi jijini Dar es salaam.
Kocha
msaidizi wa JKT Ruvu Greyson Haule alisema wapinzani wao leo wamecheza
vizuri sana lakini bahati katika mchezo huo iliangukia upande wao.
“Hakika
mchezo ulikuwa mgumu, lakini kiwango cha timu yangu kinaniridhisha siku
hadi siku licha ya kuachwa na kocha wetu Charles Kilinda, lakini sasa
tunaye mwalimu Keny Mwaisabula ambaye kiukweli kachangia mambo mengi
sana” . Alisema Haule.
Haule
aliongeza kuwa kushinda mchezo wa leo ni hatua kubwa kwao kwani
wanajipa matumaini mazuri ya kufanya vizuri mechi zilizosalia.
Kocha
huyo alisema sasa hesabu zao ni mchezo ujao dhidi ya maafande wa
Tanzania Prisons “Wajelajela” ambao wanajiandaa kunyakua mzigo wa pointi
tatu muhimu.
“Tunajiandaa
kufanya vizuri na lazima shughuli iwe nzito na Prisons, tuna morali
kubwa na mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kwasababu tuna uhakika wa
kubakia ligi kuu msimu huu”. Aliongeza Haule.
Baada
ya shughuli ya leo Taifa, hapo kesho kibarua kingine ni kati ya wekundu
wa Msimbazi Simba watakaowakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka
mkoani Pwani katika dimba la taifa.
Kuelekea
katika mchezo huo, kocha msaidizi wa klabu ya simba, Jamhuri Kiwhelo
Julio alisema wachezaji wote wapo salama na wanajiandaa kukumbana na
wanajeshi hao ambao wako sawa kwa kila idara”.
“Shooting
ni timu nzuri na kila mtu anajua, matokeo yoyote yatakayopatikana
tutamshukuru Mungu, wachezaji wanajua ugumu wa mechi lakini kocha Liwieg
kushirikiana na mimi tumefanya maandalizi kwa wachezaji wetu”. Alisema
Julio.
Julio
alisema kufungwa ni jambo la kawaida katika mchezo wa soka huku
akitolea kipigo cha jana walichokipata Barcelona kutoka kwa Bayern
Munich cha mabao 4-0.
“Jana
kila mtu alikuwa anashangaa, lakini soka ni mchezo wa mahesabu,
ukikosea unapigwa, na ndio maana jana Barca walicheza ovyo wakapigwa
kipigo cha mbwa mwizi, na sisi tukifungwa sio ajabu”. Alisema Julio.
Kocha
huyo aliwataka mashabiki wa simba kuwaombea dua njema wachezaji wao ili
waamke salama hapo kesho, lakini pia wajitokeze uwanjani kuwashangilia
vijana wao.
Kwa
upande wa Ruvu Shooting, afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire alisema
wamejiandaa kuwafunga simba wanaosikika wakisema wanataka kulinda
heshima mechi zilizosalia baada ya kupoteza ubingwa wao msimu huu..
“Tumesikia
maneno ya wana Simba kuwa wanataka kutufunga na kulinda heshima,
mwalimu Mkwasa mnamjua, kafanya mambo yake na kesho mnyama hatoki
kwetu”. Alijigamba Masau.
0 comments:
Post a Comment