Mshambuliaji nguli wa JKT Ruvu Mussa Hassan Mgunya “Mgosi” (kulia) akifanya vitu vyake katika mechi dhidi ya Yanga
Kikosi cha Prisons kinachotaraji kushuka ugani siku ya mei mosi dhidi ya JKT Ruvu
Na Baraka Mpenja
Wakichagizwa
na ushindi wa 1-0 dhidi ya Africa Lyon wiki hii, maafande wa jeshi la
kujenga taifa JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani wapo katika morali kubwa
kujiandaa na mchezo wa mei mosi dhidi ya wanajeshi wenzao kutoka jijini
Mbeya “Jiji la Kijani”, Wajelajela Tanzania Prisons uwanjwa wa Chamazi
Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo Greyson Haule ameiambia MICHEZO BOMBA!
kuwa mpaka sasa wachezaji wote wako salama, hakuna majeruhi yeyote na
wana morali kubwa kutokana na kuwepo katika mikono salama ya kusalia
ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
“Sisi
tuko makini sana, wachezaji wangu wote wako barabara, tunarekebisha
makosa madogo madogo yaliyoonekana mechi iliyopita, nadhani kufikia siku
ya mechi tutakuwa fiti kuwavaa Prisons”. Alisema Haule.
Haule
aliongeza kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu sana kutokana na timu hizo kuwa
sambamba katika msimamo, wote wakiwa na pointi 26 lakini Prisons wapo
juu yao kufuatia wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Prisons yupo nafasi ya 9 wakati Ruvu wapo nafasi ya 10 katika msimamo.
Timu
zote mbii zitaweza kusalia ligi kuu bara msimu huu kwani zina pointi
nzuri na zinaweza kujichimbia zaidi endapo zitachanga kwa uzuri karata
zao za mwishoni.
Wakati huo huo maafande wa Tanzania Prisons leo hii wapo njiani wakisafiri kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi hiyo.
Katibu
mkuu wa klabu hiyo Sadick Jumbe alisema wamefanya maandalizi ya kutosha
na wameamua kufika siku mbili kabla ya mchezo ili wachezaji wapumzike
kabla ya kipute hicho.
“Tuko
vizuri, wachezaji wote wapo salama na wana morali kubwa sana kuibuka na
ushindi, akina Elias Mguli, Sino Augostino, Henry Mwalugala, Lugano
Mwangamba na wengine wengi wote wana morali kubwa kuwaadhibu JKT Ruvu
mei mosi”. Alisema Jumbe akiwa njiani.
0 comments:
Post a Comment