Na Baraka Mpenja
Homa
ya pambano kali la masumbwi ama ndonga la kuwania ubingwa wa IBF Africa
baina ya bondia bingwa mtetezi Francis Cheka dhidi ya Thomas Mashali
“Simba asiyefugika” inazidi kupanda kwa mashabiki wa wanaume hao wenye
ubora zaidi katika mchezo huo.
Rais wa Kampuni ya ngumi za kulipwa Tanzania Yasin Abdallah “Ustadhi” ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa tayari mabondia wote wapo Dar es salaam na leo hii majira ya saa
tano asubuhi watapima uzito katika ukumbi wa hoteli ya Nzeka Magomeni
Kondoa jijini hapa.
“Hakika
tambo zimetawala kila kona huku mashabiki wa mabondia hao wakitambiana
kwa hali ya juu, leo hii tunawapima uzito na kesho shughuli yenyewe
itaanza ukumbi wa PTA kwa wapinzania hao kupanda ulingoni wakitanguliwa
na mapambano ya utangulizi”. Alisema Yasin.
Akizungumzia
vipimo vya matumizi ya kuongeza nguvu “Bangi” na mengine mengi, Yasin
alisema mabondia wote watapimwa na kama kuna bondia atabainika kutumia
madawa hayo yanayokatazwa michezoni basi atauza ushindi wake kwa
mpinzani wake.
Ustadhi
aliwaomba mabondia wote watakaocheza mapambano ya utangulizi kujitokeza
mapema ili kukamilisha zoezi la upimaji wa uzito kabla ya kuwapima
wanaume wawili watakaoshindania gari mpya aina ya Noah.
Kiingilio
cha chini katika pambano hilo litakalopambwa na mapambano mengi ya
utangulizi kitakuwa shilingi elfu saba za kitanzania (7000/=).
Yasin
alisema mashabiki wa mji kasoro bahari Morogoro wamesisitiza kuwa
hawatakubali kupoteza ubingwa wao na gari mpya, bali watamuunga mkono
Cheka mwanzo mwisho katika ili achukue tena taji hilo.
Kwa
upande wa mashabiki wa Mashali wa jijini Dar es salaam wanajigamba kuwa
bingwa wa Afrika Mashariki na Kati “Simba asiyefugika” Thomas Mashali
lazima amtandike Cheka ambaye ni mpinzani wake mkubwa kwa sasa.
Tambo
zimetawala jijini Dar es salaam huku mashabiki wengi wakimfananisha
Cheka na timu za Hispania, Barcelona na Real Madrid kuwa ufalme wake
umefika ukingoni na sasa anavua rasmi taji lake.
Kwa upande wa Cheka ameiambia MICHEZO BOMBA! kuwa amezoea maneno ya wapinzani wake, kwani waliwahi kuongea wengi lakini wakaambualia kipigo cha aibu.
“Niko
vizuri sana, nimejiandaa kwa umakini mkubwa kutetea ubingwa wangu,
mashabiki wangu wa Morogoro wananisapoti sana na sitawangusha hata
kidogo”. Alisema Cheka.
0 comments:
Post a Comment