Friday, April 5, 2013

EUROPA_LIGI_CUP>>FENERBAHCE YAICHAPA LAZIO!!
MECHI 4 za Robo Fainali za EUROPA LIGI zilichezwa jana na England, yenye Timu 3, ilipata matokeo tofauti kwa Timu zao Chelsea, Tottenham na Newcastle.
ZIFUATAZO NI TAARIFA KUHUSU MECHI HIZO:
TOTTENHAM 2 FC BASEL 2
YALE matumaini ya Tottenham kutinga Nusu Fainali za EUROPA LIGI jana yaliingia dosari kubwa baada ya kutoka sare ya Nyumbani ya Bao 2-2 na Basel ya Uswisi walipolazimika kutoka 2-0 nyuma na kusawazisha.
Uwanjani White Hart Lane, Basel walitangulia kufunga kwa Bao za haraka haraka za Valentin Stocker na Fabian Frei lakini Emmanuel Adebayor akaipatia Spurs Bao moja na kufanya matokeo kuwa 2-1 hadi Mapumziko.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2
-Adebayor Dakika ya 40
-Sigurdsson 58
Basel 2
-Stocker Dakika ya 30
-Frei 34
++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Gylfi Sigurdsson aliisawazishia Spurs na kufanya Gemu kuwa 2-2 lakini Spurs walipataka pigo kubwa pale Mchezaji wao wa kutegemewa Gareth Bale alipotolewa nje kwa Machela baada ya kuumia enka.
Bale ndie Mfungaji Bora wa Tottenham akiwa na Mabao 22 Msimu huu na tangu Januari Mosi, Tottenham hawajashinda Mechi yeyote ambayo Bale hajafunga.
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Naughton, Gallas, Vertonghen, Assou-Ekotto, Dembele, Parker, Lennon, Bale, Holtby, Adebayor
Akiba: Lloris, Dempsey, Huddlestone, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Caulker.
Basel: Sommer, Steinhofer, Schar, Dragovic, Voser, El-Nenny, Die, Salah, Fabian Frei, Stocker, Streller
Akiba: Vailati, Ajeti, David Degen, Alexander Frei, Cabral, Sauro, Zoua.
Refa: Milorad Mazic (Serbia)
CHELSEA 3 RUBIN KAZAN 1
WAKICHEZA kwao Stamford Bridge, Fernando Torres aliifungia Chelsea Bao 2 na Victor Moses Bao moja na kuipa ushindi Chelsea wa Bao 3-1 dhidi ya Rubin Kazan ya Urusi.
Bao pekee la Rubin Kazan lilifungwa na Bibras Natkho kwa Penati baada ya John Terry kuunawa Mpira.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Benfica 3
-Torres Dakika ya 16 & 70
-Moses 32
Rubin Kazan 1
-Natcho Dakika ya 41 [Penati]
++++++++++++++++
Hata hivyo, Chelsea wanajua bado wana kibarua kigumu cha kutinga Nusu Fainali katika Mechi ya Marudiano huko Moscow Wiki ijayo kwani Rubin Kazan ni wagumu wakiwa kwao na Msimu huu kwenye Mashindano haya wameshazitupa Timu ngumu wakiwemo waliokuwa Mabingwa Kombe hili Atletico Madrid na nyingine ni Partizan Belgrade, Inter Milan na Levante.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Terry, Luiz, Bertrand, Ramires, Lampard, Moses, Benayoun, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Ivanovic, Oscar, Mikel, Hazard, Ferreira, Marin.
Rubin Kazan: Ryzhikov, Cesar Navas, Kuzmin, Kaleshin, Ansaldi, Sharonov, Orbaiz, Roman Eremenko, Karadeniz, Natcho, Dyadyun
Akiba: Arlauskis, Ryazantsev, Kasaev, Kisliak, Marcano, Tore, Rondon.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
BENFICA 3 NEWCASTLE 1
Newcastle, wakicheza ugenini huko Estadio da Luz, Mjini Lisbon, Ureno, walijikuta wakisambaratika katika Kipindi cha Pili na kutwangwa Bao 3-1 na Benfica.
Papiss Cisse aliwapa matumaini Newcastle kwa kufunga Bao la kwanza kabisa baada ya pasi safi ya Moussa Sissoko lakini alishindwa kuipa Bao la pili pale shuti lake lilipopiga mwamba na mara tu baada ya hapo Rodrigo akaisawazishia Benfica.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Benfica 3
-Rodrigo Dakika ya 25
-Lima 65
-Cardozo 70 [Penati]
Newcastle 1
-Papiss Cisse Dakika ya 12
++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Cisse tena akapiga posti na Benfica wakapiga Bao la pili baada ya kuinasa pasi mbovu ya nyuma ya Beki wa Newcastle Davide Santon na Lima kufunga.
Oscar Cardozo aliipa Benfica Bao la Tatu kwa Penati baada ya Steven Taylor kuunawa Mpira.
FENERBAHCE 2 LAZIO 0
WAKICHEZA kwao, Fenerbahce walitumia vizuri mwanya wa kucheza na Mtu 10 Lazio na kufunga Bao za mwishoni na kuibuka na ushindi wa Bao 2-0.
Lazio walipata pigo baada ya Ogenyi Onazi kupewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 47 na upungufu huo uliwasaidia Fenerbahce kushinda Mechi hii.
Katika Dakika ya 79, Pierre Webo alifunga kwa Penati kufuatia Stefan Radu kuunawa Mpira na Straika wa zamani wa Liverpool, Dirk Kuyt, akafunga Bao la pili baada ya kunasa Mpira uliobabatiza Walinzi kufuatia frikiki ya Caner Erkin.
VIKOSI:
Fenerbahce: Demirel; Gonul, Yobo, Korkmaz, Ziegler; Topal, Meireles; Kuyt, Cristian, Sow; Webo
Lazio: Marchetti; Ciani, Cana, Radu, Gonzalez; Candreva, Onazi, Hernanes, Lulic; Ederson; Kozak
EUROPA LIGI:
ROBO FAINALI:
MARUDIANO
11 Aprili 2013
[Saa 1 Usiku]
Rubin Kazan v Chelsea [1-3]
[Saa 4 Dak 5 Usiku]
Newcastle v Benfica [1-3]
Basel v Tottenham [2-2]
Lazio v Fenerbahce [0-2]
NUSU FAINALI
Mechi ya 1=25 Aprili 2013
Mechi ya 2=2 Mei 2013
FAINALI
15 Mei 2013
UWANJA wa AMSTERDAM ARENA

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video