Demba Ba |
Katika dimba la darajani jijini London ni vita kali ya robo fainali ya kombe la FA nchini England baina ya wenyeji wa uwanja huo Chelsea dhidi ya vinara wa ligi kuu England, mashetani wekundu, Mnchester united majira ya saa 8 na Nusu mchana.
Wiki 3 zilizopita miamba hiyo ya soka ilikutana Old Traford na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Nusu Fainali kucheza na Man City hapo Aprili 14 Uwanjani Wembley.
ROBIN VAN PERSIE |
Msimu huu tayari Timu hizi zimeshacheza
mara mbili Uwanjani Stamford Bridge, mara ya kwanza ikiwa Mechi ya Ligi
ambayo Man United walishinda Bao 3-2 na Siku 3 baadaye walikutana kwenye
CAPITAL ONE CUP na Chelsea kushinda Bao 5-4 baada ya Dakika 120 huku Man
United wakichezesha Kikosi dhaifu.
++++++++++++++++++++++++++
VIKOSI VINATARAJIWA:
CHELSEA Cech Azpilicueta, Luiz, Terry, Cole Ramires, Mikel Oscar, Mata, Hazard Ba ++++++++++++++++++++++++++ |
MANCHESTER UNITED De Gea Jones, Evans, Ferdinand, Evra Cleverley, Giggs Welbeck, Rooney, Nani Chicharito |
Katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya FA CUP, Man United waliongoza Bao 2-0 na Chelsea kuzinduka na kurudisha Bao zote.
Kwa ajili ya pambano hili la marudiano
Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea na Man United zilipangua Vikosi vyao
kwenye Mechi zao za Ligi za Jumamosi ambazo wote walicheza ugenini na
Man United kuifunga Sunderland Bao 1-0 na Chelsea kufungwa 2-1 na
Southampton.
+++++++++++++++++++++++++
Chelsea kwenye FA CUP:
Raundi ya 3: Southampton 5-1
Raundi ya 4: Brentford 2-2
Raundi ya 4-Marudiano: Brentford 4-0
Raundi ya 5: Middlesbrough 2-0
Raundi ya 6: Man Utd 2-2
+++++++++++++++++++++++++
Man United nao huenda wakawachezesha
Wachezaji kadhaa ambao hawakucheza kwenye ushindi wao wa Jumamosi dhidi
ya Sunderland ambao ni Evra, Rio Ferdinand, Ryan Giggs, Scholes, Wayne
Rooney, Nani, Chicharito, Paul Scholes na Phil Jones.
+++++++++++++++++++++++++
Man United kwenye FA CUP:
Raundi ya 3: West Ham (a) 2-2
Raundi ya 3-Marudiano: West Ham (h) 1-0
Raundi ya 4: Fulham (h) 4-1
Raundi ya 5: Reading (h) 2-1
Raundi ya 6: Chelsea (h) 2-2
+++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, kambi zote mbili za Timu
hizi zimedokeza kuwa huenda Mechi hii ikakosa ladha hasa kwa vile
inakuja Masaa 48 tu baada ya Timu hizi kucheza Mechi zao za Ligi.
++++++++++++++++++++++++
FA CUP
RATIBA:
ROBO FAINALI-MARUDIANO:
Jumatatu Aprili 1
[SAA 8 na Nusu Mchana]
Chelsea v Manchester United
NUSU FAINALI:
WEMBLEY STADIUM
Jumamosi Aprili 13
[SAA 1 na Robo Usiku]
Millwall v Wigan
Jumapili Aprili 14
[SAA 12 Jioni]
Chelsea/Manchester United v Man City
FAINALI:
Jumamosi Mei 11
0 comments:
Post a Comment